Thursday, November 5, 2009

Miss Utalii Ilala kesho kivumbi.........!!

Baadhi ya washiriki wa Miss utalii Ilala 2009



Miss Utalii Ilala 2009 kesho tarehe 6/11/2009 Ijumaa katika ukumbi wa Da’ West Park Inn Tabata itakuwa ndio mpango mzima...!! kwani jumla ya Warembo 12 watapanda jukwaani kuchuana kuwania taji hilo.

Warembo walioanza kambi kwa takribani mwezi mmoja katika Ukumbi wa Da’ West Park Inn-Tabata, waliweza kujifunza masuala mbalimbali yanayohusiana na Utalii unaopatikana Tanzania ikiwemo Hifadhi za Utalii za Taifa, Vivutio vya Kitalii, pamoja na Maajabu ya Dunia yanayopatikana hapa Tanzania.

Aidha katika shindano hilo, warembo hao wataonyesha Mavazi ya asili ya makabila mbalimbali ya Tanzania, watacheza ngoma kuonyesha utamaduni wa Mtanzania, Watavaa mavazi ya Kitanzania ya Kitalii, vazi la Ubunifu lililotengenezwa kwa maligafi za hapa Tanzania, pamoja na mengine mengi yanayohusiana na masuala ya Utamaduni wa Mtanzania.

Warembo wanaowania taji la Miss Utalii Ilala 2009 ni pamoja na ,Tickey Lighton,Neema King’aka, Edna Endrew, Frola Nicholaus, Sheila Baamary, Janeth Samson, Nezia Gabriel, Roselina Sekwao, Jamida Abdu, Aghata Kilala, Tabus Thomas, na Shaymin Ntemena.

Zawadi mbalimbali zenye thamani ya shilingi milioni kumi zitatolewa kwa washindi ikiwa ni pamoja na Fedha, na vifaa mbalimbali vyenye thamani vitalolewa kwa washindi ambapo mshindi wa kwanza kwa mujibu wa Waandaji wa shindano hilo ni thamani ya shilingi milioni 2, mshindi wa pili thamani ya million moja na laki mbili ,mshindi wa tatu thamani ya laki nane na , mshindi wa nne na tano, thamani ya laki tano na mshindi wa Kipaji (Talent) ni thamani ya laki saba na nusu na kifuta jasho kwa wote ni shilingi elfu thelathini na watapatiwa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi laki moja kila mmoja.

Extra Bongo ya mzee wa farasi zamani, Zia musica, ngoma za asili pamoja na wasanii wa kizazi kipya

No comments:

Post a Comment