World News

Tuesday, November 17, 2009

Mjue 'Selemani Semunyu' anayepania kukuza mchezo wa Mpira wa Kikapu Tanzania...!!

Selemani Semunyu mwandishi wa habari na mtangazaji wa kituo cha redio Times fm ya jijini DSM hapo juu pichani, ni miongoni mwa wagombea wanaowania nafasi ya Kamishna ya Kamisheni ya Watoto ktk chama cha Shirikisho la mpira wa Kikapu Tanzania (TBF).

Jamaa ana skills na uzoefu mwingi ktk mchezo huu wa Basket Tanzania, kiasi cha kuweza kuibua vipaji vingi vya Mpira wa kikapu kuanzia kwa watoto wadogo na kufikia level za kina Hashim Thabeet.


Selemani Semunyu aka Super Tall alipokuwa anarudisha fomu ya kugombea nafasi hiyo ya Kamishna Kamisheni ya Watoto TBF

Uchaguzi wa viongozi wapya wa TBF utafanyika tarehe 28 Novemba ya mwezi huu baada ya kuahirishwa hapo awali.

Mdau huu ni wakati wetu kuwapigia kura viongozi wa ukweli watakao fanya mageuzi ya ukweli ktk chama cha Mpira wa Basket Tanzani (TBF) kwa miaka minne ijayo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...