World News

Tuesday, November 17, 2009

Msanii wa Bongofleva ashambuliwa kwa kisu na 'msela mavi' Kipawa Dsm....!!

Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Abraham Kassembe aka Dullayo mwishoni mwa wiki hii alikubwa na mkasa wa kuvamiwa na kushambuliwa na majamaa wa2 wakiwa na msichana mmoja kwenye taxi aliyokuwa amekodi, ambapo mmoja wao alitoa kisu na kumjeruhi vibaya mkononi wakati akijaribu kuzuia kisu hicho kilichokuwa kinaelekea mwilini mwake kwa mara ya pili.
Jamaa aliyemchoma kisu anaonekana kuwa muhuni flani ivi asiye na dira yaani 'Msela mavi' km wanavyofahamika uswahilini kwetu.

Dullayo anasema anaendelea vizuri kimtindo baada ya kupatiwa matibabu kwa usiku ule, ila alipokuwa akihojiwa na kituo cha redio Times Fm cha jijini Dar es salaam na Issa Kiango alisema pamoja na majereha hayo bado ana uwezo wa kufanya kazi zake kama kawaida, hivyo hata km kuna show ya kuimba bado ataifanya hata leo kwasababu ameumia mkono wa kushoto na Mic huwa anashikia mkono wa kulia.

Alimaliza kwa kusema anawaachia Polisi wanaoendelea na kazi yao!

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...