Moja
kati ya msanii anayefanya muziki wa bongo fleva Edson Wilison a.k.a
Baby boy ambaye alipotea kwenye game ya muziki,sasa amerudi kwa kishindo
kikali.
Baby
boy ambaye alipotea kwa kipindi kirefu, zaidi ya miaka miwili kwenye
muziki sasa amerudi na ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la Funga
Mkanda aliyofanya chini ya studio iliyopo maeneo ya sinza lego jijini
dar es salaam inaoitwa Flexible music.
Ngoma hiyo ambayo Baby Boy akiwa amemshirikisha Barnaba boy na msanii anayeitwa Shazy Melody,ambaye yupo lebo chini ya Flexible Entertainment ikiwa imetengenezwa na mtayarishaji Basmart the next hit wa studio hiyo.
Baby
Boy akizungumza kuhusu ujio wake mpya ameeleza kuwa unampa matumaini
sana na kuwaomba mashabiki wake wampokee vizuri maana ndiyo amerudi kwa
nguvu zote.
“Hii
ni ngoma yangu mpya ambayo nimefanya na Barnaba Boy na Shazy Melody na
wimbo wangu unaitwa Funga Mkanda ambayo natarajia kuiachia siku yangu ya
birthday yaani siku yangu ya kuzaliwa alhamisi ya tarehe 6 mwezi huu”
Baby Boy alisema.
Pia aliongeza kuwa ujio wake huo hautaweza kumfanya arudi nyuma tena kwenye muziki na alifafanua kuhusu ngoma hiyo
“Aaah
ni ngoma ambayo naelezea jinsi gani nimerudi maana najua mashabiki
zangu walikuwa na hamu na mimi kwa kipindi kirefu sana kama mtu
aliyekuwa na kiu jangwani”Aliongeza Baby Boy.
No comments:
Post a Comment