Mwanamuziki
Ebrahim Makunja aka Kamanda Ras Makunja mtunzi,mwimbaji kiongozi wa
bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma africa band aka FFU
Ughaibuni yenye makao yake nchini Ujerumani, amefunguka na machache
yafuatayo kuhusu mabadiliko ya katiba mpya ya Tanzania na haki za raia
wa Tanzania:
Akizungumza kutoka katika makao yake mjini Oldenburg,Ujerumani.
Kamanda Ras Makunja wa kikosi kazi FFU-Ughaibuni alisema
Kuwa: MCHAKATO WA KATIBA MPYA UMEWAFANYA WATANZANIA
WENGI KUSOMA KATIBA YA ZAMANI ! MWANZO WALIKUWA HAWAISOMI NA KULIELWA VEMA !
WENGI KUSOMA KATIBA YA ZAMANI ! MWANZO WALIKUWA HAWAISOMI NA KULIELWA VEMA !
Kwa sasa ! WATANZANIA HATUNA HAJA YA KUOGOPA MAUMIVU YA
MABADILIKO YA KATIBA LAZIMA TUENDE KUFUATANA NA WAKATI,
LAZIMA TUWEKE MASALAHI YA TANZANIA NA MTANZANIA KWANZA,
Ras
Makunja,alichambua zaidi kwa kusema kuwa watanzania tumekuwa tunatabia
za uwoga wa maumivu ya mabadiliko linapokuja swala la kujadili masilahi
ya kitaifa na mtanzania,mara nyingine bila ya kujijua tunawapigania
watu ambao sio walengwa katika katiba "Nina maana walengwa wa
kunufahika katika katiba hii lazima wawe watanzania wote wa bara na
visiwani ambao wanaishi popote pale duniani" bila kujali dini,jinsia au
vyama vyao vya kisiasa.
SWALI: NINI ? MTAZAMO WAKO NA UNATARAJIA NINI ? KATIKA KATIBA MPYA ?
RAS.MAKUNJA:
Mtazamo wa wangu katika kulijadili hili la katiba mpya ningewaomba
kwanza wale wabunge walio katika bunge maalumu la katiba
kwamba : WAFANYE KILA HALI KATIKA MJADALA HUU KUPATA KATIBA
YENYE MASILAHI 99% TANZANIA NA MTANZANIA KWANZA
YENYE MASILAHI 99% TANZANIA NA MTANZANIA KWANZA
Mfano: Haki za kumiliki Ardhi,tunapoongelea swala la Haki ya mtanzania
basi Ardhi na maslahi yanayo patikana katika Ardhi lazima yamilikiwe na
raia
wa Tanzania kwanza,kwa sababu Ardhi ndio msingi au ubongo wa nchi
yetu,kwa maana hii asilimia kubwa ya ardhi kama haipo katika miliki ya
raia
wa Tanzania ,uhuru wetu unatakuwa umepungua maana.
ARDHI NA RAIA WA TANZANIA NDIO MOYO WA TAIFA NA UTAWALA
WA TANZANIA,asilimia 50% ya Adhi ikiwa mikononi mwa watu ambao sio
WA TANZANIA,asilimia 50% ya Adhi ikiwa mikononi mwa watu ambao sio
watanzania,au watu ambao wana offer za kukaa au kufanya jambo katika
ardhi kwa mktaba wa miaka mingi ,wananchi tutajikuta tupo ugenini
katika ardhi yetu.HII HAINA MAANA KUWA TUNAWAFUNGIA MILANGO WAWEKEZAJI
BALI TUNAWEZA KUINGIA NAO MIKATABA YA MUDA MFUPI .
RAS MAKUNJA: SIO SWALA LA WENGI WAPE ! NA WACHACHE WANYIME BALI SWALA LA HAKI YA BINADAMU NA URAIA
WATANZANIA LAZIMA TULITAZAME SWALA URAIA PACHA KWA FAIDA YA TANZANIA NA PIA TULICHAMBUE HASARA NA FAIDA ZAKE.
Ras Makunja aliingia kwa kina kwa kusema kuwa kuhusu uraia pacha
walio wengi wanahitaji kuelemishwa faida na hasara zake,pamoja na haki
za msingi kwa watanzania wanaomba hili liwemo katika katiba mpya.
Kwanza tunapolizungumzia hili lazima tujue nini ?maana uraia na nini maana Pasipoti.
Historia inaonyesha kuwa matumizi ya PASIPOTI yalianza mapema mwaka
1910 SOVIET UNION (URUSI) ndio walioanzisha kwa nia ya kuwathibiti raia
wao katika mfumo wa kikomunisti,baada ya hapo ndipo madola mengine yakafuata;
Leo tunapoongelea uraia pacha wengine wanachanganya pasipoti tu za kusafiria na kusahau haki za uraia na binadamu kwa ujumla.
Katika kanuni za haki za binadamu hairuhusiwi mtu kunyang'anywa uraia wake,
Mimi ningeshauri kuwa katiba mpya iruhusu raia watanzania waweze
kuwa na pasipoti zaidi ya tatu,kwa sababu zitawasaidia katika maswala la
maendeleo,kama vile uchumi,elimu n.k
MFANO HAI KUNA WATOTO
WALIOZALIWA NJE YA NCHI WAZAZI WAO WOTE NI WATANZANIA LAKINI WANAKOSA
HAKI KATIKA NCHI WALIOZALIWA KWA KUWA SI RAIA WA NCHI HILE,NA
WANAPOTIMIZA MIAKA 18 WANASHINDWA KUUKANA URAIA WA TANZANIA NA KUOMBA WA
NCHI WALIOZALIWA JAPO NCHI WANAYOISHI WANAWEZA KUWA RAIA PACHA.
Watoto hawa wanasulubiwa kwa kuhukumiwa makosa ambayo hawajafanya !
kwani awakuomba wazaliwe ughaibuni,watanzania katika katiba mpya lazima
tuwafikirie watoto hawa wasio na hatia.
Hata katika kanuni za
haki za binadamu zinasema kuwa "Si ruhusa kwa binadamu yeyote yule
kunyanga'nywa uraia wake.Sasa mtoto wa kitanzania
akiwa hana haki ya kuwa mtanzania kwa kuwa kazaliwa nje ya nchi ! hii si haki.
(B)
Muwekezaji wa Kigeni anapokaribishwa Tanzania kwa maneno ya "Jisikie
upo Nyumbani ! na mtanzania hakubaliki kwao hapa kidogo pana utata
lazima patazamwe upya.
Kwa sasa kuna nchi nyingi duniani ambazo katika
katiba zake zinasema kuwa raia wa nchi hizo harusiwi kuny'angwa uraia
wake ata kama anaomba uraia wa nchi nyingine,sisi bado tunaogopa
kulijadili kwa visingizio vya usalama.
Kwa Sasa hatuna adui kama ilivyokuwa zamani tuliofu makaburu n.k
Adui wetu wa sasa ni NJAA NA UMASIKINI na Uraia pacha unaweza kuwa silaha kubwa ya kupiga vita adui zetu hawa NJAA,UMASIKINI.
TUNAWEZA KUWEKA MASHARTI KWA WALE WATAKAO KUWA NA URAIA PACHA(Ras Makunja alisisitiza)
Mfano: Mtu akiwa na uraia pacha hawezi kugombea nafasi za juu ya uongozi wa taifa kama vile mbunge,diwani,rahisi.
Au kufanya kazi katika sekta ya usalama na mambo nyeti yanayo husu taifa.
huu ni mfano tu. Uraia pacha si swala la kuliogopa bali kuelimishana.
SWALI : MATEGEMEO YAKO ? KUHUSU KATIBA MPYA.
Ras Makunja: Ni mategemeo yangu kuwa wabunge katika bunge
maalumu la katiba wataweka maslahi ya Tanzania na watanzania kwanza na
kuondoa itikadi zao za ki-vyama kama tunanyoona sasa. Tunategemea
watatuletea rasimu ya mapendekezo ya katiba yenye masilahi ya Taifa na
watanzania kwanza
si vinginevyo. mwanamuziki huyo alimalizia.
No comments:
Post a Comment