MWENYEKITI
wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta amewatoa wasiwasi wasanii wa
Tanzania wakati alipokutananao jana Bungeni mjini Dodoma kwalengo la
kuwasikiliza wasanii hao wakiwa na kilio chao cha kusahaulika kwa kipengele kinachohusu
Haki Miliki (Intellectual Property) za kazi za wasanii katika Rasimu ya Katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mhe.
Sitta mesema kuwa nidhahiri kuwa Katiba iliyopo sasa imepitwa na wakati kwani haigusii
mambo mengine yakiwemo hakiya vitu visivyoshikika kama vile haki hizo za wasanii
na wagunduzi hapa nchini.
“Tunachojaribu
kufanya hapa Dodoma ni kutunga Katiba ambayo nirafiki kwa kila Mtanzania ili iweze
kumsaidia kila mmojakatika eneo lake, hivyo hii itakuwa ni Katiba iliyorafiki”.
Alisema Mhe. Sitta.
Aidha,
Mhe. Sitta amewapongeza wasanii wote 25 waliowawakilisha wenzao kwakuja Bungeni
mjini Dodoma kwaajili ya kuwasilisha mapendekezo yao iliyaweze kutambuliwa kwenye
rasimu hiyo.
Wasanii
hao ambao wamefuatana na viongozi wao wa msafara, pia amewapongeza kwa kazi kubwa
na nzuri waifanyayo wasanii wengi wa Tanzania katika kuitangaza nchi yao.
Naye
Mkuu wa msafara wa wasanii hao, ambaye ni Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania
(TAF) Bw. Simon Mwakifwamba amemueleza Mhe. Sitta kuwa kuna umuhimu wa Katiba Mpya
itakayopatikana ihakikishe inalinda Haki Miliki za wasanii pamoja na utambuzi wakundi
kubwa la wasanii ndani ya Katiba hiyo kwani ndiyo wanafanyakazi kubwa ya kuitangaza
Tanzania ndani na nje ya mipaka yake.
“Wasanii
wanafanya kazi kubwa ya kuitangaza nchi ambapo kwasasa takwimu zamchango
wao, katika
Pato la Taifa kwa mujibu wa ripoti ya mwaka 2013 ya Chama cha Haki
Miliki cha Kimataifa kwa kipindi cha mwaka 2007hadi mwaka 2010 sanaa
zote imechangia
kwa asilimia 4.3% zaidi ya madini, gesi, maji na hoteli, na tasnia ya
sanaa imetoa
ajira kubwa kwa zaidi ya asilimia 5.6%, hivyo naomba katika Katiba Mpya
kuwepo nauungwaji
mkono wa wasanii hasa katika kulinda Haki Miliki zao (Intellectual
Property).
Kwaupande
wake MakamuMwenyekiti wa Bunge hilo,Mhe. Samia Suluhu Hassan aliwashukuru wasanii hao, kwa kufika Bungeni na
kuja na jambo zuri lenye manufaa kwa wasanii na Taifa kwa ujumla na amewahakikishia
kuwa maombi yao ya kutaka Katiba Mpya ilinde Haki Miliki za kazi zao ya tafanyiwa
kazi.
“Kuja
kwenu Dodoma katika shughuli hii kunaonyeesha jinsi mlivyo na upeo , hili ni jambo
la msingi kuwekwa katika Rasimu ya Katiba. Huu ni wakati pekee wakuhakikisha
mambo yenu yanatambulika,” alisemaMhe. Samia.
No comments:
Post a Comment