Pages

Monday, October 13, 2014

MATOKEO MISS TANZANIA 2014 'UTATA' MTUPU!!!

Kamati ya Miss Tanzania ikiongozwa na Lundenga ndio yenye dhamana ya kutangaza matokeo ya mshindi wa taji la mrembo wa Tanzania baada ya majaji kufanya kazi yao. Ndio maana lawama na malalamiko yote juu ya Utata na ubatili wa matokeo anatupiwa bwana Lundenga na kamati yake

Dhahiri ilionekana kabisa na wadau wanaofatilia mashindano kuwa yaliyotangazwa pale ukumbini hayakuwa matokeo halali juu ya miss Tanzania 2014 ndio maana ukumbi mzima haukurithishwa na matokeo yale isipokuwa kikosi fulani kilichokuwa upande wa mshindi Sitti Mtemvu

Majaji 9 wakitafakari matokeo ya miss Tanzania yaliyotangazwa

Hali hii inachangia sana mporomoko na mvuto wa mashindano haya kama tunavyojionea.

Hakika mashindano ya urembo Tanzania yamepoteza msisimko, na ni kuanzia ktk ngazi ya vitongoji ambapo tunaona uchache wa wapenzi wanaohudhulia ktk maonyesho hayo sehemu mbalimbali. 

Pia ushiriki wa warembo umekuwa wa tabu sana wengi wakiogopa kupoteza muda wao sababu ya maana halisi ya mashindano imeshapotea kwa kuwa washindi tayari wanakuwa wamepangwa hivyo imani imewatoka kabisa.

Hata wadhamini wa mashindano hayo wamepungua sana (sababu hayavutii tena wadhamini) na wengi kutojitokeza kabisa kiasi cha kufanya mashindano kutoFana na upatikanaji wa zawadi kuwa tabu kwa waandaaji hasa kwenye mashindano ya awali.

Mashindano ya Miss Tanzania ni moja kati ya mashindano makubwa sana hapa nchini ikiwa yamefanyika kwa mara 20 sasa tokea mwaka 1994, lakini SASA yamepoteza umaarufu na heshima yake kutokana na UTATA wa matokeo sehemu mbalimbali, hata wapenzi wake hawana tena imani.......Pengine kungekuwa na KURA za wazi labda km BSS.......ama utaratibu ubadilike........au kamati imechoka......

No comments:

Post a Comment