Ndani ya
mwezi ujao wa Kumi na Moja (November) Tarehe 2 itakuwa ni siku yenye Neema
kwani Arusha Kutashushwa Baraka ya Kumthamini na kumuonyesha Upendo Mama Wa
Kitanzania na Duniani Kote.
Hadi sasa
Maandalizi ya Tamasha la Upendo kwa Mama Yamekamilika ambapo Tarehe 2 November
2014 Ndani ya Viwanja vya Sheikh Amri Abeid Kutafanyika tamasha hilo lililobarikiwa jina la UPENDO KWA MAMA ambapo Tamasha
hilo litaongozwa na waimbaji wa Nyimbo za Injili
wakubwa kutoka humu Nchini na Nchi Jirani ya Kenya.
Wasanii
hao wa Injili Watakaoongoza Tamasha la UPENDO KWA MAMA Sara K kutoka Nchini
Kenya na Cristina Shusho kutoka Tanzania, huku likipambwa na Ambwene Mwasongwe,
Baraka Maasa, Eng calros Mkundi, Ester Bukuku, Matha Mwaipaja, Nesta sanga,
Meth Chengula, Matumaini, Eline Patrick bila kuwasahau waimbaji wengine kutoka
Mkoani Arusha pamoja na Kwaya Mbalimbali.
Lengo hasa
la tamasha hilo la UPENDO KWA MAMA ni kutoa Mitaji kwa zaidi ya akina mama 50
wajasiriamali ili kuwaongezea uwezo wa kujiajiri, vilevile utakuwa ni wakati
mwafaka wa kuwashukuru wakinamama wote kwa upendo walionao ukiambatana na
kujitolea katika kusimamia Familia na malezi ya watoto.
Kama
Mtanzania au Usiyekuwa Mtanzania mwenye Mapenzi na mama Basi unaalikwa Kufika
katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha Tarehe hiyo na utashuhudia Tamsha hilo kwa Kuchangia
Kiingilio Kidogo tu ambacho ni Sh. 3,000/= (Elfu Tatu ya Kitanzania)
Tamasha
la UPENDO KWA MAMA limeandaliwa na Mkundi Production ya Jijini Arusha na
wao kama kamati ya maandalizi ya
Tamasha la UPENDO KWA MAMA wanatoa nafasi kwa watanzania, Taasisi na Mashirika
yote ambayo yako tayari kuungana na Studio ya Mkundi kwa Ufadhili wa hali na
mali ili kufanikisha tamasha hili la UPENDO KWA MAMA.
No comments:
Post a Comment