Akiwa ana nyimbo za “Mwana” na “Kimasomaso” zikiongoza katika vituo mbali mbali Africa, Alikiba
aachia video ya “Mwana” iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu jana ,Ijumaa tarehe 19
Decemba 2014 kwa mamilioni ya mashabiki Africa na duniani. “Mwana” ni nyimbo ya
kwanza baada ya kufunga mkataba wake na
kampuni ya Rockstar4000 Management na Rockstar Publishing.
Rekodi ya “Mwana” ni nyimbo ya kwanza kutoka
kwenye albamu ya tatu ya Alikiba baada ya kutokuwa katika muziki kwa muda wa
miaka mitatu. Alikiba alifafanua kwa kusema “ Hii ni album itayoonyesha kukua
kwangu kimuziki na kuonyesha utofauti mbali mbali katika kipaji changu
nilichojaliwa.”
Alikiba alitoa kibali ili video ya “Mwana”
iruke hewani jana “exclusively” kwa masaa 24 kwenye vituo vya televisheni
vitano Africa katika vipindi maarufu kwenye vituo hivyo na kuwafikia mashabiki
zaidi ya milioni 500 kwa pamoja. Vituo vya televisheni hivyo ni Clouds TV
kuonyesha exclusive Tanzania, Nation TV kuonyesha exclusive Uganda,
One Music Networks kuonyesha exclusive Cameroon, Angola, Ethiopia, USA
na UK, Sound City kuonyesha exclusive Nigeria na Ghana na Citizen TV
exclusive kwa upande wa Kenya, DRC Congo na Rwanda
Mashabiki wanaweza kuangalia video ya “Mwana” katika Youtube channel
yake Alikiba au hapa
Au kwa kupitia mitandao yake ya kijamii.
Video ya “Mwana” itaendendelea kuruka kwenye vitu vingine mbali mbali Africa na duniani leo
Alikiba’s
official website: www.IamAlikiba
Bookings: officialalikiba@gmail.com
Facebook: www.facebook.com/rockstar.alikiba
Twitter: @OfficialAlikiba or twitter.com/officialalikiba
Instagram: @OfficialAlikiba or instagram.com/officialalikiba
No comments:
Post a Comment