Uvaaji wa nguo zilizochanwa chanwa au kuwekwa vilaka kwa makusudi
unaojulikana kwa jina la "Midabwada's Style" unazidi kuwatia wazimu
vijana hususan vijana wa kisasa aka Dotcom Generation
hawaoni wala kusikia mbele ya vazi la midabwada,
mtindo wa vazi hilo sio
kitu kipya bali katika historia inaonyesha katikati ya miaka 1960s hadi
mwishoni mwa miaka 1970s jamii ya vijana wa enzi hizo katika nchi za
ulaya ya magharibi na Amerika haswa vijana wa kizungu walianzisha
harakati na kujiita Hippie au Hippy Movement ambao wengi
wa vijana hao walitoka katika familia na wazazi matajiri mno lakini
vijana hao wakawa na mavazi yenye kuchanika ,vilaka vilaka na pengine
kutembea bila ya kuvaa viatu ili mradi waonyeshe kuwa wapo
katika hali duni au sawa na masikini.
Lakini katika enzi hizo pia
kulikuwa na harakati za vijana watanashati wenye kujipenda na kupenda
utanashati wengi wao walikuwa miongoni mwa wamerekani weusi au wenye
asili ya afrika hao mpaka mitindo yao ya nywele ni Afro do.
Katika miaka hii kuwepo kwa midabwada's Style ni kurudia mitindo hile hile sema
kinachozidi ni zile mbwembwe na Swagaz ..lazima ujue jinsi ya
kudundika Midabwada's Style..tena vazi hili lina bei ya juu sana sana
huko ulaya Jeans moja ya Midabwada's inafikia mpaka Euro 120= sawa na
Tsh.240,00= usichangae mzazi kumununulia mwanao jeans mpya kesho
ukaikuta Midabwada's, hapa bongo mtindo huu unasemekana ulianzishwa na
mgonjwa wa akili chizi kejeli ambaye ni marehemu...hakuna uhakika.
Stori na Zainab Ally Khamis
No comments:
Post a Comment