Friday, September 18, 2009

Madaraka Nyerere awaasa wabongo kuupanda mlima Kilimanjaro..!!


Mtoto wa Raisi wa1 wa Tanzania Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere Bw. Madaraka Nyerere anatarajia kuanza kupanda Mlima Kilimanjaro Septemba 29 hadi oktoba 6 mwaka huu pia ataongozana na mtoto wa Raisi wa zamani wa Uganda Bw. Jaffar Idd Amin ambapo atakuwa akimuunga mkono ktk adhima yake hiyo ya kuupanda mlima.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo) Dar es salaam jana, Bw. Madaraka alisema kuwa watatumia siku nane kupanda na kushuka mlima huo.

"Lengo la kupanda Mlima Kilimanjaro ni kupata fedha kusaidia watoto yatima wapatao 200 wa kituo cha community Alive kilichopo kuweza kuwapatia mahitaji muhimu kama chakula na sare za shule". Bw. Madaraka amesema.

Alisema lengo la pili kupanda mlima huo ni kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kwa mambo mazuri ambayo aliyafanya katika uhai wake pia ni sehemu ya kumbukumbu ya maadhimisho ya Miaka kumi tangu kufariki kwake.


Pia mapema asubuhi alisema wakati wa kupanda mlima ukifika kule juu unakutana na watu wengi sana wengi wao wakiwa wageni kutoka nchi za nje, unaweza kufikiri labda uko ugenini!! hii inaashiria watanzania wengi hawapandagi mlima Kilimanjaro mlima mrefu kuliko yote Afrika, Tujitokeze kupanda mlima Kilimanjaro isiwe kwa watalii tu wanaotoka nchi za kigeni.....!

No comments:

Post a Comment