Thursday, September 24, 2009

Nyimbo mpya kutoka Iringa......


Ngoma ya msanii wa bongofleva 'IBRAH' anayewakirisha pande za Iringa imeingia leo kunako Playlist ya Makavulive, Isikilize mdau....Nyimbo inaitwa 'Chocolate' imetengenezwa na Producer mkali ambaye pia ni presenter wa Redio 'Country Fm' ya mjini Iringa Temmy Mahondo aka 'Temmy G' pichani hapo juu.

Hii sio ngoma ya kwanza kutengenezwa na Producer Temmy G, mchizi kesha piga mikono kwenye ngoma kibao zikiwemo za wasanii waishio Dar km Dullayo, Ommy G na wengine, pia nyimbo mpya ya Dullayo 'Naumia Roho' ambayo inafanya vizuri sasa jamaa ndie aliyeanza kuitengeneza ktk studio ya Iringa Dullayo alipoenda kupiga-show miezi michache iliyopita kabla ya Kisaka na KGT.

ISIKILIZE MDAU AF TUONE....... ipo no. 4 kwenye Playlist hapo mwanzo kulia!!!

No comments:

Post a Comment