Na Mwandishi Wetu
WAREMBO wanaotarajiwa
kushiriki shindano la Miss Dar Intercollege 2012 jumamosi hii wanatarajiwa kutembelea
makumbusho ya Taifa kwa ajili ya kujifunza.
Shindano hilo linatarajiwa kufanyika katika ukumbi huo
wa Makumbusho ya Taifa uliopo mkatabala na chuo cha usimamizi wa Fedha (IFM)
Juni, 22 mwaka huu.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, mratibu wa shindano hilo
Dina Ismail, alisema ziara hiyo itawasaidia sana warembo hao katika harakati zao za
kielimu.
Alisema Makumbusho ya Taifa
ni sehemu muhimu kwa kila Mtanzania kufahamu kutokana na kuwepo vitu vingi vya
kihistoria vilivyopata kutokea katika karne zilizopita.
“ Kama
mjuavyo kule kuna kuna fuvu la mtu wa kwanza duniani (zinjathropas), vyombo,
magari na vitu vingine vya kwanza kuanza kutumika,”alisema.
Dina aliongeza kuwa
maandalizi kwa ajili ya shindano hilo
yanakwenda vema ambapo washiriki 13 kutoka vyuo vya IFM, Ustawi wa Jamii, Chuo
Cha Biashara (CBE), uandishi wa Habari (DSJ) na Huria (OUT) wanaendelea na
mazoezi kwenye hoteli ya The Grand Villa iliyopo Kijitonyama jijini Dar es
Salaam.
Warembo hao ambao wapo chini
ya ukufunzi Marlydia Boniface na Bob Rich ni pamoja na Veronica Ngota, Rose Muchunguzi,
Nancy Maganga, Hilda Edward, Diana
Nyakisinda, Neema Michael, Veronica Yollla, Jacquiline Cliff, Sharifa Ibrahim,
Natasha Deo, Saada Suleiman, Rose Masanja na Jamila Hassan.
Shindano hilo limedhaminiwa
na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia kinywaji cha Redd’s Original, Dodoma
Wine, Ndege Insurance, Shear Illusions, Skylight Band, Lamada Hotel, Screen
Masters, Makumbusho ya Taifa, Mustafa Hassanali, Grand Villa Hotel, Clouds Fm
na blog za Michuzi, Mamapipiro, Bin Zubeiry, Mtaa kwa Mtaa na Full Shangwe.
No comments:
Post a Comment