Tisho Boy (Muhindi Kutisha) ni msanii chipukizi wa kizazi kipya
mwenye uwezo wa kuimba na kufoka(Rap) ambaye pia ni Mwanafunzi wa
Computer Engineering Nairobi Kenya.
Alianza sanaa ya uimbaji akiwa
chekechea wakati huo akishiriki katika kwaya ya shule. Swala la uimbaji
halikuwa limechipuka sana kwani maigizo yalimchukuwa muda sana. Alipenda
ushairi na fasihi kwa ujumla na haswa mwanzo wake, tungo za kishairi
akazifanya nyimbo.
Wimbo wake wa kwanza Mpenzi Nakupenda
aliomshirikisha 2M, haukumfurahisha lakini ikawa changamoto chanya kwake
kama kawaida ya wasanii chipukizi wanapochupuka.
Alifwata na Nipe Flow
ambao amemshirikisha Farisayo(Emmanuel Karisa) pamoja na Lidwati na Tuna
akimshirikisha Farisayo vile vile ambazo amezifanyia UGC (Orynx Music)
Production, Kenya kwa mitindo ya Kapuka/Genge. Anatazamia
kufanya video hivi karibuni.
Tisho
Boy ni Mwandishi pia wa Riwaya na Tamthilia. Riwaya yake 'Kumbukumbu za
Kutisha' anaitazamia kuipiga chapa na matbaa mojawapo nchini Kenya. Pia
yeye hutunga na kughani mashairi na vilevile anakusudia kutoa Diwani
yake ya Mashairi 'Kabwela la Bara' mwakani.
Alizaliwa 1990, Desemba 23 nchini Kenya. Asili yake ni ya Kitaita na Kihaya.(Bongo)
Anapenda
muziki, kucheza na kutazama soka, shabiki mkubwa wa Chealsea, kutazama
Bongo Movie na ana ndoto ya kufanya Bongo Movie siku za halafu. Ana
uraibu na maswala ya tarkalishi sana na kuimba.
Farisayo |
Tuna_Tisho Boy ft Farisayo.
Tuna
ni wimbo ulioimbwa kwa mtindo wa ragga/Dancehall/Kapuka. Ni Klub song
ambayo inazungumzia kula bata haswa walengwa wakiwa vijana na yeyote
mwenye uwezo wa kujirusha. Ina maudhui ya starehe ya klub na
pia inakashifu wenye jicho na chuki. Kwani wapende wasipende,
tunajirusha. Imefanywa UGC Production na Producer Miwo nikimshirikisha
Farisayo( Emmanuel Karisa)
http://www.reverbnation.com/open_graph/song/13545738, Unaweza kuskiza na Ku-download free nyimbo hii ktk Playlist ya Makavulive hapo juu.
Nipe Flow
Nipe
flow ni track ambayo ina maudhui ya mapenzi. Kuna binti nampenda lakini
kuna wenye kijicho wenye wivu. Nawakausha kwa track hii kwa kumwambia
binti huyu anipe flow nizidi kuringa(Kujiroll)
No comments:
Post a Comment