Omary Mubba aka Ommy G, msanii kitambo wa Hiphop Tanzania ameamua kumrudia Mwenyezi Mungu 'MOLA' baada ya kimya kirefu kutotoa wimbo wowote wa Hiphop. Akiongea na Makavu blog Gangsta amesema 'unajua huu muziki tunaofanya kiukweli hauruhusiwi ila tunafanya tu kwa ajili ya fedha na vitu kama hivyo'.
Amesema amefanya nyimbo ya Hiphop inayoitwa "Mola nisamehe" ktk Studio za Emotion chini ya usimamizi wa Prodyuza Kisaka akimshirikisha 'Salu B' na muda wowote kuanzia sasa utaskika ktk vituo vya redio.
Ommy G anasema ameamua kumwimbia Mungu ili kuwakumbusha kwamba Mwenyezi Mungu yupo pia anawakilisha jamii ambayo imemsahau Mungu, muziki unakazi ya kuelimisha na kuburudisha ila sasa imekuwa-too much maana kila msanii akiimba anaimbia Pombe na wanawake na hivyo nyimbo zao zinachochea Ongezeko la maasi duniani, na kupotosha maadili ya ki-Afrika.
Ommy G hivi karibuni aliachia nyimbo mbili za 'Hiphop Mdundiko', "Wambele mbele" na "Mtoto wa nyumba ile" ambapo nyimbo moja kati ya hizo ilikuwa-Nominated ktk Tuzo za muziki Tanzania japo hakufanikiwa kushinsa Tuzo hizo.
No comments:
Post a Comment