Bia ya Redd's premium imetoa udhamini wa sh. milioni 200 ktk kinyang'anyiro cha kumsaka mnyange wa Tanzania, akizungumza Dar es Salaam leo Meneja wa Redd's Kabula Nshimo alisema wao na Kampuni ya Lino wameingia mkataba wa miaka mi3 wa kuwa mdhamini mwenza wa mashindano hayo, pia Samsung ni mdhamini mwingine wa mashindano hayo yatakayofanyika Oktoba 2 mwaka huu pale Milimani City.
Alisema mashindano ya mwaka huu hayatakuwa na balozi wa Redd's isipokuwa kutakuwa na mashindano ya kumsaka Miss Photo Genic atakayepatikana kupitia issamichuzi.blogspot.com na kwamba mshindi huyo atafanya kazi anazotakiwa kufanya balozi wa Redd's.
No comments:
Post a Comment