World News

Thursday, June 9, 2016

XXL AFRO SUMMER JAM, 30TH JULY

COME AND JOIN US TO FEEL THE SPIRIT & RHYTHM OF AFRICA!!!
Save the date:
30. July 2016 - Kultur Arena, Stuttgart
### XXL AFRO SUMMER JAM, 1st EDITION ###
with an incredible concept that is going to turn the crowd on:
# The Ngoma Africa Band live on stage
# Top DJ's from BigFM & Afro Moves
# Dance show performances
# Fantastic arena
# And many more....
ALL YOU CAN GET FOR ONE EVENING.
Get your ticket now!
(xxlafrosummerjam@gmx.de // +49(0)157-32161521)
https://www.facebook.com/events/1536043496703545/?ti=icl

Wednesday, June 1, 2016

MISS CHANG'OMBE 2016 INATAMBULISHWA KESHO 'MPOAFRIKA' - DAVIS CORNER

KAMPUNI ya SG Entertaiment imewataka warembo kutoka kata zote zilizopo chini ya chang'ombe wenye sifa na vigezo stahiki kujitokeza bila kuogopa  kuchukua fomu za kushindani wa Miss Chang'ombe.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mratibu wa mashindano hayo Adam Hussein,  alisema uzinduzi wa uchukuaji fomu hizo zitaanza kuchukuliwa kesho kutwa  saa 2:00 asubhi na kutarajiwa kuisha Juni 5 mwaka huu eneo la CDS Park (TCC Club) Chang'ombe, Mpo Afrika Davis Kona na duka la nguo la Chilu Latest Wear.

Mratibu wa Mashindano ya Shindano la Miss Chang'ombe, Adam Hussein, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kuhusiana na kutaka Kuzinduliwa kwa Mashindano ya Urembo Miss Chang’ombe Juni 2 Mwaka huu. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano katika Shindano hilo, Victor Mkumbo
"Miss chang'ombe rasmi itazinduliwa,kesho katika ukumbi wa Mpo Afrika uliopo Davis Corner Tandika, hivyo tunaomba mtupe ushirikiano kuja kushiriki ili kuweza kukuza tasnia hii ya urembo" alisema Hussein.


Mkuu wa kutengo cha habari kutoka kampuni hiyo Victor Mkumbo, alisema vigezo vinavyotakiwa kwa washiriki hao ni kuwa na cheti cha kuzaliwa au kadi ya kupigia kura, kitambulisho cha taifa ili kuweza kuepusha udanganyifu unaojitokeza mara kwa mara.
"Baadhi ya washiriki watakao shiriki ni Neema Ogote(20), sitizuhura Husein (20), Hadija Salumu(18), Anitha Mugisha (19), Dorothea Shayo (20), Anba Mtua(20), Rehema Mongi (21), na Esther  Mnahi(22), kutoka Wilayani Temeke" alisema.

Alisema fainali ya mashindano hayo yatafanyika Julai 21 mwaka huu katika viwanja vya CDS Park, ambavyo zamani vilijuwa vikitwa TCC Club Chang'ombe jijini Dar es Salaam.

Uzinduzi huo utasindikizwa na wasanii kibao akiwepo MSAGA SUMU, CHEMICAL, GALATONE na wasanii wengine Kibao huku mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Diwani wa Kata ya Tandika 

NGOMA AFRIKA BAND YATAJWA KUWA BENDI IMARA BARANI ULAYA


Ngoma Africa band imetajwa ni bendi hiliyovuka dhoruba na kushika chati ulaya kianzo kimoja maarufu cha habari barani ulaya AFRONEWS kimeitaja
bendi hiyo kuwa imejijengea ngome imara na kuwashika washabiki wa
kimataifa kisawa sawa soma zaidi bofya link chini

How Ngoma Africa Band has survived the storm to become one of the most sought-after African bands in Germany http://www.afronews.de/entertainment/ngoma-africa-band-survived-storm-become-one-sought-african-bands-germany/

Monday, May 2, 2016

NGOMA AFRICA BAND YAWATAKIA HERI YA SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI


Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa Band aka FFU-ughaibuni au viumbe wa ajabu Anunnaki aliens inayoongozwa na mwanamuziki mashuuri Ebrahim Makunja aka Kamanda Ras Makunja inaungana na wadau wote wa habari duniani kwa kuwatakia kila la heri na baraka wanahabari na vyombo vyao kwa kusherehekea siku ya Uhuru wa Habari duniani.
 
Bendi inaungana na wadau wote wa habari kwa wimbo maalumu wa "Uhuru wa Habari" utunzi wake kamanda ras Makunja.
Sikiliza song: Uhuru wa Habari

Thursday, April 14, 2016

"KING-KONG" Cjamoker ft Wakazi_Ibrah_P the Mc_One the Incredible_Zaiid(Offici

MTINDO WA VAZI LA MIDABWADA'S STYLE INAZIDI KUWATIA WAZIMU VIJANA

Uvaaji wa nguo zilizochanwa chanwa au kuwekwa vilaka kwa makusudi unaojulikana kwa jina la  "Midabwada's Style" unazidi kuwatia wazimu vijana hususan vijana wa kisasa aka Dotcom Generation hawaoni wala kusikia mbele ya vazi la midabwada, 
 
mtindo wa vazi hilo sio kitu kipya bali katika historia inaonyesha katikati ya miaka 1960s hadi mwishoni mwa miaka 1970s jamii ya vijana wa enzi hizo katika nchi za ulaya ya magharibi na Amerika haswa vijana wa kizungu walianzisha harakati na kujiita Hippie au Hippy Movement ambao wengi wa vijana hao walitoka katika familia na wazazi matajiri mno lakini vijana hao wakawa na mavazi yenye kuchanika ,vilaka vilaka na pengine kutembea bila ya kuvaa viatu ili mradi waonyeshe kuwa wapo katika hali duni au sawa na masikini.
 
Lakini katika enzi hizo pia kulikuwa na harakati za vijana watanashati wenye kujipenda na kupenda utanashati wengi wao walikuwa miongoni mwa wamerekani weusi au wenye asili ya afrika hao mpaka mitindo yao ya nywele ni Afro do.

Katika miaka hii kuwepo kwa midabwada's Style ni kurudia mitindo hile hile sema kinachozidi ni zile mbwembwe na Swagaz ..lazima ujue jinsi ya kudundika Midabwada's Style..tena vazi hili lina bei ya juu sana sana huko ulaya Jeans moja ya Midabwada's inafikia mpaka Euro 120= sawa na Tsh.240,00= usichangae mzazi kumununulia mwanao jeans mpya kesho ukaikuta Midabwada's, hapa bongo mtindo huu unasemekana ulianzishwa na mgonjwa wa akili chizi kejeli ambaye ni marehemu...hakuna uhakika.
 Stori na Zainab Ally Khamis

Rest In Peace NDANDA KOSOVO!!

1977 - 2016
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...