KAMPUNI
ya SG Entertaiment imewataka warembo kutoka kata zote zilizopo chini ya
chang'ombe wenye sifa na vigezo stahiki kujitokeza bila kuogopa
kuchukua fomu za kushindani wa Miss Chang'ombe.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mratibu wa mashindano
hayo Adam Hussein, alisema uzinduzi wa uchukuaji fomu hizo zitaanza
kuchukuliwa kesho kutwa saa 2:00 asubhi na kutarajiwa kuisha Juni 5
mwaka huu eneo la CDS Park (TCC Club) Chang'ombe, Mpo Afrika Davis Kona
na duka la nguo la Chilu Latest Wear.
Mratibu wa Mashindano ya Shindano la Miss Chang'ombe, Adam Hussein,
akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kuhusiana na
kutaka Kuzinduliwa kwa Mashindano ya Urembo Miss Chang’ombe Juni 2 Mwaka
huu. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano katika Shindano hilo, Victor Mkumbo.
"Miss
chang'ombe rasmi itazinduliwa,kesho katika ukumbi wa Mpo Afrika
uliopo Davis Corner Tandika, hivyo tunaomba mtupe ushirikiano kuja
kushiriki ili kuweza kukuza tasnia hii ya urembo" alisema Hussein.
Mkuu
wa kutengo cha habari kutoka kampuni hiyo Victor Mkumbo, alisema vigezo
vinavyotakiwa kwa washiriki hao ni kuwa na cheti cha kuzaliwa au kadi
ya kupigia kura, kitambulisho cha taifa ili kuweza kuepusha udanganyifu
unaojitokeza mara kwa mara.
"Baadhi
ya washiriki watakao shiriki ni Neema Ogote(20), sitizuhura Husein
(20), Hadija Salumu(18), Anitha Mugisha (19), Dorothea Shayo (20), Anba
Mtua(20), Rehema Mongi (21), na Esther Mnahi(22), kutoka Wilayani
Temeke" alisema.
No comments:
Post a Comment