Tuesday, July 5, 2016

USAJILI WA "KARATE CLUB OF JUNDOKAN SO HONBU SYSTEM TANZANIA" NI NEHEMA

Sensei Rumadha Fundi, wakiwa na Sensei Pedro Cardeira toka Lisbon, Ureno wakifanya zoezi la mbinu ya kuvunja mkono


Habari za uhakika zimetufikia kuwa chama cha Karate club of Jundokan So Honbu System Tanzania kimepata usajili.Tanzania itasonga mbele na kushika nafasi za kimataifa baada ya usajili huo kwani Mkufunzi mkuu au Chief instructor wa chama hicho anayetambuliwa kimataifa na baraza la dunia la karate la dunia lenye makao yake Okinawa Japan Sensei Rumadha Fundi, mwenye uzoefu wa vyama vitatu vya Goju Ryu tofauti, pia, alithibitisha hayo baada ya kupata msaada  mkubwa chini ya watu walio karibu sana nae ambao pia imekuwa ni nguvu kubwa inayo mpa moyo wa kuwa na mfumo huo asilia toka visiwa vya Okinawa, Japan.
Jundokan So Honbu, ni mfumo unaofundisha mtindo wa Okinawa Goju Ryu katika utamaduni na utaratibu uliyowekwa na Master Chojun Miyagi na kusambazwa na mwanafunzi wake ambaye ni mwanzilishi wa JUNDOKAN, Master Eiichi Miyazato 1957, huko wilaya ya Asato,mji wa Nana, katika kisiwa cha Okinawa, Japan.

Maana ya Jundokan " Sehemu ya mafundisho us mwanzilishi"JUN +DO+ KAN, "jun"ni imekuchuliwa toka jina la mwanzilishi wa Goju Ryu, Chojun  na "Do" ikimaanisha mwenendo, " Kan" ikimaanisha shule au mafunzo.
Hivyo ndivyo hasa lengo kuu la mfumo huu asilia usio badilishwa au kugeuzwa jinsi unavyofundishwa tokea ulipo undwa na Master Miyagi.
Mipango ipo njiani kuwa na tawi lenye lengo na nia kufuata sheria na kanuni za mfumo asilia tu, bila kubadilisha mbinu na "Kata" kama jinsi inavyo bainika na mbinu za " Sports Karate" hasa uchezaji wa "kata" kiujumla.
 
Hivi karibuni, huko visiwani Okinawa katika makao makuu ya tawi hilo, jumuiya ya sanaa ya mapambano " Okinawan BUDOKAN & Karate Federation", imeitambua "Jundokan So Honbu" kama moja ya mitindo asili"Original" kutoka Okinawa inayozingatia maadili na mafunzo yaliyo achwa na mua sisi wa mtindo wa Okinawa Goju Ryu.
Pindi mnamo miezi ijayo, tutatoa taarifa ya ufunguzi rasmi wa shule ya karate na uteuzi wa wanafunzi wa kuu wasaidizi ambao Sensei Rumadha atajitoa muhanga kuwasaidia kimbinu na ubora wa umahili wa mtindo huu na kuhakikisha mnamo muda wa miaka michache wanapata fursa ya kuwa walimu ( sensei) na kusambaza JUNDOKAN SO HONBU Tanzania yote.
"Msingi tunao mzuri na imara kwa wengi wataojumuika nami kuendeleza hii sanaa hapa nyumbani Tanzania", alisema Sensei Rumadha mwenye uzoefu wa mafunzo hayo ya karate zaidi ya miaka 37 chini ya " ma-sensei" wakuu toka pande zote za  dunia, hasa toka Okinawa, Japan,Alimalizia hayo.
 
 Na Zainab Ally Hamis (DSJ)

No comments:

Post a Comment