World News

Thursday, February 4, 2010

Dullayo kuwatoa " THE PROMISE"..!!

The Promise

WASANII chipukizi wa kundi la muziki wa kizazi kipya nchini 'The Promise, wamemaliza kurekodi nyimbo nne mpya kwa ajili ya maandalizi ya albamu yao ya kwanza.


Kiongozi wa kundi hilo, Abdalah Kilima 'Kilima' alisema kuwa kundi hilo linaundwa na wasanii watatu ambao ni Willium Salvatory 'AS', Hassan Mohamed 'Hans' pamoja na yeye.


Alisema kuwa wamemaliza kurekodi nyimbo hizo katika studio ya K .Records ambapo baadhi ya nyimbo zimeshaanza kufanya vyema katika baadhi ya stesheni za redio.


Kilima alisema kuwa kundi lake linatarajia kutoa albamu yao ya kwanza mapema mwaka huu ambayo wanatarajia itakuwa na jumla ya nyimbo 10.


"Tumeshamaliza kurekodi nyimbo tatu hivyo tunajipanga kukamilisha taratibu za kurekodi nyimbo nyingine kwa ajili ya kukamilisha albamu yetu ya kwanza" alisema Kilima, nyimbo hizo ni Nyakolema waliyomshirikisha Dullayo na Kigwema, Narudi Nyumbani, Si Unanikumbuka na Love.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...