Monday, June 28, 2010

BABU AYUBU azindua album ya CHAJA YA KOBE jana...!

Msanii mahiri Mc Babu Ayoub usiku wa jana amezindua album yake ya taarab ktk ukumbi wa Traverntine Magomeni jijini DSM.
Huku akisindikizwa na wasanii kibao tofauti tofauti km Diamond anayeimba bongofleva, Hadija Kopa mamaa wa mipasho, Banza Stone na wengine kibao Babu Ayub alikonga nyoyo za mashabiki wake na kuonyesha kweli Taarab imemkubali kuliko alipokuwa akifanya Bongofleva ambayo anasema hailipi, amezindua rasmi album hio yenye nyimbo 4 ambazo ni 'Chaja ya kobe', 'Jipu la Kwapa' n.k.
Mpangomzima wa show hio uliandaliwa na mwanadafada mahiri ktk tasnia ya Taarab Tanzania, Khadija Shaibu aka DIDA wa Times Fm chini ya DD&G Entertainment ikipewa shavu na duka kubwa la kuuza nguo za kijanja la Dida Classic Boutique lililopo Kinondoni na kinywaji cha Redd's Premium

No comments:

Post a Comment