KATIBU Mkuu wa klabu ya AShanti United ya jijini Dar es salaam Haji Bechina kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa michezo wamepanga kuwaombea dua marehemu wote waliowahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi wa klabu hiyo itakayofanyika katika shule ya msingi Boma Ilala jijini Dar es salaam
Bechina aliwataja watakaosomewa duwa hiyo kuwa ni pamoja aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Tabora, Ukiwaona Ditopile Mzuzuri aliyekuwa Mlezi wao Rajabu Mgodo, Athumani Nobi waliokuwa makatibu katika vipindi tofauti na Mzee Mwalimu Kinyogori ambaye alikuwa mwenyekiti.

Bechina alisema kuwa klabu zote za mpira wa miguu zilizopo jijini DAr es salaam pamoja na wadau wa mchezo wa soka wamepewa mialiko kwa kushiliki dua hiyo itakayofanyika jumapili hii ya julai 25
Aidha klabu hiyo imepanga kuisuka upya timu ya soka ya AShanti United baada ya kupoteza mwelekeo miaka ya hivi karibuni.
Mbali na soka AShanti pia hujishughulisha na uinuaji wa vipaji vya mchezo wa ngumi kupitia kocha Rajabu Mhamila Super D
Bechina aliongeza kuwa wanajivunia timu hiyo ya ngumi ambako mchezaji wao Joseph Richard, alimpiga kwa KO ya raundi ya pili Kijepa Omari katika pambano la utangulizi kabla ya Rashidi Matumla na Mada Maugo kwenye ukumbi wa P.T.A, ndani ya viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam
No comments:
Post a Comment