CHAMA cha haki miliki Tanzania (COSOTA) kimezuia kupigwa kwa wimbo wa msanii chipukizi wa Bongo Fleva Mwingereza Athuman ‘Tanzanite’, ujulikanao kama ‘Kafara’, imefahamika.
Hatua hiyo inafuatia chipukizi mwingine wa bongo fleva, Nassib Abdul ‘Diamond’ kupeleka mashitaka cosota akidai kuwa Tanzanite amenakili wimbo wake wa ‘Mbagala’. Tanzanite ambaye pia anajulikana kama Abuu Flava alisema kabla ya kurekodi wimbo huo aliongea na Diamond na kumuomba kufanya hivyo, alimkubalia lakini anashangaa baada ya kutoka akaenda kushitaki Cosota.
Alisema licha ya Diamond kuitwa katika vikao vya usuluhishi cosota alikuwa hatokei na mwishowe maamuzi yakatolewa, hata hivyo anasema amekubaliana na maamuzi hayo na hana kinyongo chochote.
Tanzanite alisema kilichofanya Diamond ageuke ni baada ya kuona ‘Kafara’ ni mzuri kuliko ‘Mbagala’ ndiyo maana ameingiwa na hofu, lakini hata hivyo amejipanga kikamilifu katika medani ya muziki na anatarajia kutoa nyimbo bomba zaidi.
Maamuzi ya COSOTA ni kama yafuatavyo.........
1. COSOTA watatoa matangazo kwa FM Radio zote kupiga marufuku wimbo wa KAFARA usichezwe tena!
2.Itabidi Abuu Flava amlipe fidia msanii Diamond kama akitaka.
No comments:
Post a Comment