Thursday, July 8, 2010

Matumla, Maugo kuzichapa Julai 18 PTA Sabasaba....!

Mjasiriamali wa mpambano wa ngumi, Selemani Semunyu katikati akiwa na mabondia Rashidi Matumla (kushoto) na Mada Maugo wakati wa kutangaza mpambano wao wa kirafiki utakaofanyika julai 18

BONDIA mkongwe wa ngumi za kulipwa nchini, Rashid Matumla 'Snake Man', anatarajia kuzichapa na mpinzani wake Mada Maugo 'Junior', katika pambano lisilokuwa la ubingwa litakalofanyika Julai 18 mwaka huu, kwenye Ukumbi wa PTA, Sabasaba Dar es Salaam.Akuzingumza na waandishi wa habari jana, Rais wa Oganaizesheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania'TPBO', Yassin Abdalah 'Ustaadh' alisema kuwa mabondia hao wanatarajia kupanda ulingoni Julai 18 mwaka huu.

Alisema kuwa pambano hilo la uzito wa Middle lenye raundi 10, linatarajiwa kuwa na upinzani mkali kutokana na historia za mabondia wote.Abdalah alisema kuwa wameamua kuandaa pambano hilo ili kutoa burudani safi kwa wadau na wapenzi wa mchezo wa ngumi nchini.

Alisema kuwa pambano hilo limeandaliwa na Kampuni ya Media Entertainment & Sports Promotion na linaratibiwa na TPBO.

No comments:

Post a Comment