Saturday, July 3, 2010

Tuwa-support Wasanii na wanamichezo waingie Bungeni 2010 na serikalini, wakatusemee...!

Baadhi ya wasanii wamejitosa ktk ulingo wa siasa, mi naona kwamba wametoka ktk jukwaa la kufikisha ujumbe kupitia mziki sasa wamehamia jukwaa kuu ambalo Serikali inaweza kuskiza kwa uzuri zaidi mambo mbalimbali wanayoshauri sasa ikiwa ni live kabisa, yaani bila ya kutumia beats/mdundo... lets support them!!

Mwana-Hip Hop mwanaharakati mkubwa Bongo, Kalama Masoud ‘Kalapina’ alijitosa kwenye ulingo wa kisiasa ikiwa ni pamoja na kuweka wazi azma yake ya kugombea Udiwani wa Kata ya Kinondoni, Dar.

Alisema:-

“Nawaomba wananchi wenzangu waniunge mkono ili tuendeleze harakati, muziki kama kawaida siachi, nitafanya siasa na muziki pamoja. Ijulikane kuwa sikuingia kwenye siasa kwa kukurupuka, bali naijua, pia wazee wamenishauri nigombee kwa sababu nakubalika sana kwenye kata yetu,”


“Nagombea kwa tiketi ya CUF, mimi ni mwanachama wa CUF tangu mwaka 1999. Nataka nimpumzishe diwani wa sasa Michael Lupiana kwasababu siasa ya siku hizi inahitaji vijana wenye uwezo wa kusimamia mambo, kujenga hoja, kubuni na kutekeleza masuala yenye manufaa kwenye jamii, sifa ambayo mimi ninayo.”


Juzikati naye Sugu aka Joseph Mbilinyi aka Mr. II alijitosa mzimamzima kunako jukwaa la siasa kupitia CHADEMA akiwa na azma kuu ya kugombea Ubunge jimbo la Mbeya mjini


hapa Sugu anaonekana akichukua fomu ya kuomba kugombea ubunge kwa tiketi ya Chadema


Tutegemee na wasanii wengine kutoka vyama vingine hususan CCM wakichukua fomu za kugombea uongozi ktk siasa!

Nimesoma leo habari ya kua presenta wa TBC 'Mai' kuwa na nia ya kugombea ubunge wa viti maalum, safi mamii........
Tumuhenzi AMINA CHIFUPA, aliyekuwa mbunge kijana akitokea ktk tasnia ya sanaa

Governor wa California Arnold Schwarzeneggar

No comments:

Post a Comment