
KUNDI la muziki wa kizazi kipya la Big Dog Pose 'BDP', linatarajia kufanya
onesho la wazi la 'Usiku wa Kino' litakalofanyika kesho katika Uwanja
wa Mtambani, Kinondoni.
onesho la wazi la 'Usiku wa Kino' litakalofanyika kesho katika Uwanja
wa Mtambani, Kinondoni.
Wilfred Mwashubila 'Drezy Chief' kiongozi wa kundi hilo amesema kuwa winatarajia kufanya onesho la aina yake kwa ajili ya kulitambulisha kwa mashabiki wake.
Kundi hilo ambalo liliwahi kutamba katika miaka ya nyuma kwenye medani ya muziki wa kizazi kipya, linatarajia kurudi upya kama ilivyokuwa zamani.
Ktk onesho hilo, pia kutakuwa na burudani kutoka kwa wasanii
mbalimbali wa Wilaya ya Kinondoni.
Big Dog Pose, linatarajia kuingiza sokoni albamu yake mpya inayokwenda kwa jina la Mtu Mzima yenye jumla ya nyimbo 12 walizozirekodia katika studio mbalimbali.
Nyimbo zilizopo katika albamu hiyo ni pamoja na Kona Zote, Kwa
yeyote, Neng'eneka, Tulifinye Para, Rudi Mpenzi Rimix, Mama Usilie, Baby, Imo, Jiskie, Huku Pia ni Kwetu na Sikuwa Hivi.
No comments:
Post a Comment