
Tarehe 1 Desemba 1988 ndipo Siku ya Ukimwi Duniani ilipoanza ikiwa na lengo kuu la kuongeza fedha, kuongeza uelewa, kupambana na chuki na kuboresha elimu juu ya hili janga.
Siku ya Ukimwi Duniani 2010 inababe ujumbe wa Universal Access and Human Rights'.
Siku ya Ukimwi Duniani ni muhimu kwa ajili ya kukumbushana kuwa virusi vya ukimwi VVU bado vipo sana, na kwamba BADO kuna mambo mengi ya kufanyika ili kujikinga.
Kulingana na makadirio ya UNAIDS, sasa kuna 33,300,000 kwa watu wanaoishi na virusi vya ukimwi, ikiwa ni pamoja na watoto milioni 2.5. Mwaka 2,009 watu milioni 2.6 wamepata maambukizi mapya na wastani wa watu milioni 1.8 walikufa kutokana na UKIMWI.
Idadi kubwa ya watu na VVU na UKIMWI wanaishi katika nchi zenye kipato cha kati. Lakini VVU leo ni tishio kwa wanaume, wanawake na watoto katika mabara yote.
Blog yako ya Makavu inaomba kila mmoja kuongea/kukumbushana na mwezio yeyote yule si lazima awe mpenzi wako juu ya janga hili Kubwa
No comments:
Post a Comment