Afisa Uhusiano wa Kampuni ya AURORA Security, (kushoto) akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu pambano la ngumi za kulipwa kati ya Awadh Tamim na Ashraf Suleiman litakalopigwa Machi 3 mwaka huu katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, kulia ni bondia Ashraf Suleiman
BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Ashraf Suleiman anatarajia kupanda ulingoni kuzichapa na Awadh Tamim katika pambano la kuwania ubingwa wa Afrika Mashariki litakalopigwa Machi 3 mwaka huu katika Ukumbi wa Diamond Jubilee.
Afisa Uhusiano wa Kampuni ya AURORA, Shomary Kimbau amesema kuwa Ashraf na Awadhi wanatarajia kuzichapa Machi 3 mwaka huu, pambano hilo litakuwa la raundi 10 katika uzito wa Heavy ambapo watakuwa wanagombania mkanda wa Afrika Mashariki na Kati ambapo kwa sasa unashikiliwa na Awadh.
Amesema kuwa pambano hilo linatarajiwa kuwa na upinzani mkali kutokana na maandalizi pamoja na rekodi za mabondia hao.
Katika pambano hilo pia kutakuwa na pambano linginea la ngumi za mseto litakalowahusisha mabondia David Mlope ´Zolla D´ pamoja na Swedy Wilson ´Kiza Kinene´ ambalo litakuwa la raundi tano katika uzito wa Heavy, pambano hilo pia kutakuwa na mapambano ya utangulizi ambayo yatashirikisha mabondia mbalimbali.
mapambano ya utangulizi, yatawakutanisha mabondia Suleiman Said dhidi Vs Maneno Osward katika pambano la raundi 10 la uzito wa Middle,
Benson Mwakyembe Vs Mbaruku Kheri katika pambano la uzito wa Light Heavy la raundi 10.
Amour Mzungu Vs Ramadhan Kiddo katika pambano la uzito wa Cruiser la raundi 10
na Alphonce Mchumiatumbo Vs Chukub Dusso katika pambano la raundi sita.
´´Tunatarajia kuona ngumi za aina yake na kuweza kupata bingwa wa Afrika Mashariki na Kati wa mchezo wa ngumi ambapo linasimamiwa na Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPRC)´´ alisema Kimbau.
Sikiliza track ya HOI kwenye playlist ya Makavulive hapo juu ambapo ZOLA D alishirikiana na OMMY G, NGUCH P pamoja na CANNIBAL SHUTTER kutoka KENYA
Sikiliza track ya HOI kwenye playlist ya Makavulive hapo juu ambapo ZOLA D alishirikiana na OMMY G, NGUCH P pamoja na CANNIBAL SHUTTER kutoka KENYA
No comments:
Post a Comment