Tuesday, March 22, 2011

SIMANZI kubwa Wasanii Tanzania..


Kijoti akitumbuiza enzi za uhai wake

Ajali mbaya iliyotokea jana barabara ya Morogoro kuelekea DSM ktk mbuga ya Mikumi na kupoteza wasanii 13 wa kiundi la Five Star Taarab akiwamo kiongozi wao Issa Hassan "Kijoti" imetia Simanzi kubwa hasa kwa wasanii na wapenzi wengi wa muziki..
wengine waliokufa ni pamoja na;Husna Mapande,Hamisa Mipango,Tizo Mgunda,Sheba Juma,Rama Kinyoya,Nasoro Madenge,Omari Tall,Fembe Juma, Hamisa Omary, Omari Hashimu na Maimuna Makuka aka kisosi wa kitu T
Huu ni msiba mzito sana ukichukulia wasanii wengi kufariki kwa mara moja ktk ajali, siku chache nyuma pia tulipata msiba wa msanii wa hiphop 'Pacha EZZY' kuchomwa kisu na kufariki jijini Arusha

DUNIA MAPITO JAMA
TUWAOMBEENI KWA MUNGU WALIOKUFA WAENDE SALAMA
NASI TUPO NJIANI HATUJUI SIKU YETU LINI
INATUPASA TUISHI KWA AMANI NA UPENDO DUNIANI


INNALILAH WAINNA ILAHI RAJIUN!!!
MUNGU WALAZE PEMA PEPONI WASANII WOTE WALIOTUTOKA

No comments:

Post a Comment