Friday, March 4, 2011

Super D kuachia Video ya kuwafundisha mchezo wa ngumi vijana Tanzania!

KAVA YA VIDEO YA SUPER D BOXING COACH

BONDIA wa Zamani na Kocha
wa Ngumi wa Klabu ya ngumi ya Ashanti, Rajabu Mhamila'Super D' yupo mbioni kutoa Video inayozungumzia maisha yake ktk mchezo huo.

Super D alisema video hiyo itakuwa sokoni kuanzia MARCH 12 ikizungumzia maisha yake tangu alipoanza kucheza mchezo huo mwaka 1984 hadi sasa.
Alisema Video hiyo itaonesha mapambano mbalimbali aliyocheza na dhidi ya mabondia Mbwana Matumla, Rashidi Ali na Ajibu Salumu.

Alisema lengo la kuandaa video ni kutaka kutimiza malengo yake ya kuendeleza mchezo wa ngumi kwa kuwapatia vijana nafasi ya kujifunza kupitia kwake. Alisema kutokana na nchi ya Tanzania kuwa na vipaji vingi atashindwa kuwafikia kila mmoja wao na badala yake amewapa fursa ya kujifunza kwa kuangalia video.
Alisema katika kuhaikisha Video hiyo inafanya vizuri sokoni ameongezea vionjo vingine kutoka kwa mabondia maarufu duniani kama Mike Tyson, Michael Mo, Junior Myweather, Mohamed Ally, Man Paqyao na Joe Fleizer

No comments:

Post a Comment