Wakati wabunge wa CHADEMA wanatolewa nje ya ukumbi wa Bunge.....Mbunge wa Mbeya mjini kwa tiketi ya Chadema, Joseph Mbilinyi, a.k.a Mr II, amelilipua jeshi la Polisi nchini kwa kashfa. Akichangia mjadala kuhusu bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani, Mr. II alieleza kashfa za jeshi hilo alizoziona wakati akiwa mahabusu ya kituo kikuu cha Polisi, Mbeya. Mr. II alizitaja kashafa hizo kuwa:
Askari polisi 2 kuwekwa mahabusu moja na watuhumiwa wengine jambo ambalo ni hatari kwa maisha yao
Wanafunzi wa chini ya umri wa miaka 18, wakiwa na sare zao za shule kuwekwa mahabusu na watu wazima
Wagonjwa 2 wa akili kuwekwa mahabusu moja na watuhumiwa
na
Mwisho kubwa kuliko, mtuhumiwa wa kizungu kutokuwekwa mahabusu kama wengine, badala yake kutengewa ofisi na kufanywa ndiyo mahabusu yake, na zaidi ya hilo kupewa na 'house girl' wa kumuhudumia ambaye ni askari wa kike wa jeshilo. Kosa lake ni kukutwa na shehena kubwa ya pembe za ndovu!!

No comments:
Post a Comment