Baada ya kura nyingi sana kupigwa na utafiti wa kina kufanyika Duniani juu ya mambo kibao yanayostaajabisha yakiwamo milima, mabonde, mito, maporomoko, mapango na kadhalika... Organisation inayoitwa Seven Natural Wonders imeteuwa vivutio 28 duniani kote ambavyo hutembelewa sana na watilii, ili vipigiwe kura na kuwa New Seven Natural Wonders of The World.
Kutoka Afrika kumechaguliwa vituo viwili tu, ambavyo ni Mlima Kilimanjaro wa Tanzania na Mlima Meza wa South Afrika. Ktk nafasi zote 28 Afrika tunagombania kuwepo ktk hizo nafasi 7 kwa kutumia nafasi mbili tu
Wadau tuonyeshe Uzalendo wa Kupiga KURA nyingi sana kwa Mlima KILIMANJARO, wenzetu wa Afrika ya Kusini tayari walishaanzisha na website ya kupromote zoezi hilo sijui kwa Tanzania kama wamefanya hivyo
ila kupiga kura unapiga moja kati ya hizi namba za simu +23 9220 1055
+1 869 760 5990
+1 649 339 8080
+44 758 900 1290
Alafu baada ya mlio ingiza namba 7716, hapo utakuwa umepiga kura moja kwa Tanzania
Fanya hivo mdau, Wazungu wako lesi ile mbaya na mwisho wa kupiga kura ni Novemba mwaka huu na Maajabu 7 mapya yatatangazwa tarehe 11.11.2011
HAYA SHIME
No comments:
Post a Comment