Friday, September 9, 2011

NAS Bizness; Msanii na Mtayarishaji wa mziki anayekuja kwa kasi

Jina kamili jamaa anafahamika kama Jonas Steven aka NAS Bizness, ni producer wa muziki ktk Studio za Pamoja Records zilizopo Kinondoni jijini Dar es Salaam. Mchizi alianza kutengeneza beats na kufanya mautundu ktk mixing kitambo kidogo akipitia ktk Studio mbambali za hapa Bongo kabla ya kupata dili ya kurekodi na kufanya mixing ktk kanisa moja pande za Nairobi Kenya

Moja ya Kazi nzuri alizozifanya ni pamoja na ngoma mpya ya kina Dullayo, Joslin, Mon G na XDizo (Makavulive) inayoitwa "Mambo mambo" ambayo tayari imeshaanza kuchezwa ktk vituo mbalimbali vya redio. Pia NAS-B amefanya kazi kibao zilizopo ktk Album mpya ya 20 PERCENT km "Zali zalina" na nyingine kibao, "Narudi kijijini" ya BEST NASA, "Binadamu" ya Peace Maker na ngoma za NEY wa Mitego.

Utapata kuskia pia ngoma mpya kutoka kwa Dullayo inayoitwa "Nimeamua" ambayo Nas B yuko mbioni kuimalizia Mixing ikiwa ktk beat kali la mtindo wa ki-south.




Kwa Upande wa pili Nas B ni msanii wa Bongofleva na tayari ameshaachia tracks kadhaa ktk vituo mbalimbali vya redio. Kuna nyimbo amefanya na 2O Percent inayoitwa "Ngombe wa Maskin Azai", 'Dua la Kuku" na nyinginezo

Weekend hii NAS B anatarajia kuanza kwa utengenezaji wa Video ya nyimbo yake mpya 'Dua la kuku" ambapo atashoot video hio ktk viunga vya Sinza pande za Palestina.

No comments:

Post a Comment