World News

Saturday, February 18, 2012

SAD News kutoka kwa familia ya XDIZO, Dada yake mzazi amefariki leo asubuhi!

'Xdizo' kushoto akiwa na mshkaji wake 'Baghdad'

Msanii wa Hipohop Bongo na mkali wa Freestyle XDIZO aka Renne Jr. amefiwa na Dada yake mzazi Erika Renne leo asubuhi nyumbani kwao Ukonga Madafu.

Kwa mujibu wa Xdizo, marehemu alisumbuliwa na maradhi ya muda mrefu, jana alipelekwa hospitalini na kupata nafuu lakini ilipofika mishale ya saa tano leo asusubuhi alifariki dunia.

Mpaka sasa Maiti imehifadhiwa ktk Hospitali ya AMANA na taratibu za Mazishi zinaendelea ambapo zitakapo kamilika tutawataarifu tena wadau.

XDIZO aliwahi kuandika nyimbo inayoitwa "Dhahabu zililizopotea" miaka na nyuma kidogo baada ya kufariki Baba yake mzazi, na leo tumepoteza dhahabu nyingine tena!

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI, AMINA!!

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...