Wednesday, April 25, 2012

AFANDE SELE ASHUKURU KUFIKISHA MIAKA 36 NA KUTIMIZA NDOTO ZAKE!!


Ujumbe wa BIRTHDAY kutoka kwa Afande Sele The'King


Shukrani zangu kwa Mwenyezi Mungu, Wazazi wangu, Family yangu, 
Mh; Joseph Mbilinyi (Sugu), Ghetto BoyZ, Watupori, Producers, wadau wa
media zote, wana morogoro, fans wangu, na artist (musician) wote wa
Afrika Mashariki

Katika miaka 36 (24-4-1976- 2012), ameniwezesha kutimiza ndoto yangu ya kutumia kipaji changu katika kuelimisha jamii,
siku zote naamini katika haya


"Fungua kinywa chako kwa ajili ya mtu asiyeweza kusema, ili kutetea
watu wote wanaopitilia mbali, Fungua kinywa chako kutetea mtu mwenye
kuteseka na umasikini"


Kupitia hayo/wao nimeweza kuwa na Album Nne Ambazo ni MKUKI MOYONI,
DARUBINI KALI, NAFSI YA MTU na HESHIMA,
album ya tano KINGDOM wakati wowote kuanzia sasa itakua sokoni, na Kuwa KING OF RHYEMES IN TANZANIA (BONGO) HIPHOP/FLAVOUR.

Kama tunasheherekea siku ya kuzaliwa, basi tukumbuke kuna siku ya kufa
vilevile, siku ya kuzaliwa iwe changamoto kwetu sote kwa kutathimini
sababu za uwepo wetu duniani, na kusudi la muumba kutuumba wanadamu,
na si wanyama, ndege, wadudu au samaki.

Lakini pia tujifunze kuwa maisha (kuishi) ndio zawadi kubwa na ya
pekee aliyotupa Muumba wetu. Tuyatunze maisha yetu na ya wengine kwa
kutenda Haki bila kikomo, na kusameheana, hakuna alie mkamilifu. MUNGU
AWABARIKI.

Asanteni.. 
SELEMANI ABDALLAH JUMA MUTABHAZI MSINDI.

No comments:

Post a Comment