Thursday, October 11, 2012

KAMANDA MGENI RASMI PAMBANO LA NGUMI MANZESE, NYERERE DAY!!

Kamanda wa Polisi mkoa wa kipolisi wa Kinondoni Charles Kenyela anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika pambano la kuwania Ubingwa wa Afrika Mashariki na kati baina ya  Thomas Mashali wa Tanzania na Medi sebyala wa Uganda Utakaopigwa Jumapili Oktoba 14 friends Corner Manzese
Akizungumza na waandishi wa habari Mratibu wa mpambano huo unaosimamiwa na oganaizesheni ya Ngumi za kulipwa nchini TPBO Regina Gwae amesema mbali kenyela kutakuwa na wageni wengine maalum akiwemo mbunge wa Kinondoni Iddi Azan
Alisema tunashukuru kwa ushirikiano wa viongozi hao katika maandalizi na hatuimaye wamethibitisha ushiriki wao katika pambano hilo ambalo linavuta hisia za watu wengi an wapenzi wa ngumi jijini Dar es Salaam.
Pia alitaja kuwa na mapambano manne ya utangulizi  ambapo Abdul Awilo atapamnana na Shedrack Juma, selemani shaaban atapambana na Hamisi Mohamed  Jonas Segu atapambana na Ibrahim Class wkati Charles mashali atapambana na Teacher Aron.
“Tumeamua kuchukua mabondi kutoka katika vilabu vyenye mashabiki wengi tumechukua kwa mzazi tumechukua klabu ya manzese anakotoka mashali na Super  D Boxing Club alisema Regina.
Regina amesema  Bondia Medi Sebyala wa Uganda na mwalimu wake wanatarajiwa kuwasili hapa nchi tarehe 11 na tayari maandalizi ya safari yao yamekamilika ikiwemo kuwatumia tiketi na tayari wameshazipokea.
Regina alishukuru kampuni ya Promasidor wasambazaji wa SOSSI Poa, Gazeti la Jambo leo,City Sports Lounge na Times Fm kwa kuwa bega kwa bega kuhakikisha pamnano hili linafanikiwa na kusema milango bado iko wazi kwa wadau kujitokeza kufanikisha mchezo huo ambao ni chanzo cha ajira kwa vijana.

No comments:

Post a Comment