World News

Saturday, November 17, 2012

MON G na TATU KUACHIA NYIMBO MPYA NOVEMBA 23!!

MSANII anayechipukia kwa kasi katika tasnia ya muziki wa bongo Fleva, Ally Ramadhan 'Mon G' pamoja na Tatu Bujashi wanatarahjia kuachia nyimbo zao mpya siku ya Ijumaa tarehe 23 ya mwezi Novemba.


Wakizungumza kwa nyakati tofauti wasanii hao, wamesema kuwa wanatarajia kuachia nyimbo mpya kila mmoja ambazo zitaingia sokoni siku moja.

Mon G aliiambia MAKAVU BLOG Dar es Salaam jana kuwa anatarajia kuachia wimbo wake mpya ambao unakwenda kwa jina la "Na Wewe" ambayo ameirekodia katika Studio ya Revange Production chini ya mtayarishaji Jumsa The One.
Mbali ya wimbo huu mpya MON G alishawahi kufanya nyimbo kama Damu Yangu, Mtoto wa Dar, na Uko Wapi aliyomshirikisha Dullayo.
Alisema kuwa baada ya kuachia wimbo huo, pia anatarajia kuitambuliusha video yake hivi karibuni ili kutoa fursa kwa mashabiki wake kupata burudani safi.

"Nimeshakamilisha wimbo wangu mpya ambao unakwenda kwa jina la Na Wewe ambayo itaanza kusikika hivi karibuni ambapo baada ya kuachia wimbo huo, ninatarajia pia kuitambulisha video yake mpya kwa masahabiki ambapo  ambapo ni projecti mpya tofauti na ile iliyozoeleka aliyofanya na Salu B ya Jipange, alisema.

"Huu wimbo ambao nautoa sasa ni wa pili ktk kukamilisha albumu yangu ukiachilia mbali zile zingine ambazo nilishirikiana na wenzangu katika project ya pamoja" alisema Mon G.

Wakati huohuo msanii wa kike chipukizi anayejulikana kwa jina la Tatu Bujash atatambulisha wimbo wake mpya unaoitwa Taratibu, uliofanywa katika studio za UB Records na mtayarishaji Star Jay.

Alisema kuwa huo ni wimbo wake wa pili tangu alipotoa wimbo ulioitwa Thank you Dj, kutoka katika studio za G Records na prodyuza KGT Shadee.

Wasanii hao wakiwa wamelamba shavu la kufanya kazi chini ya usimamizi wa kampuni ya burudani ya SG (SG Entertainment Co.)  ya  Dar es salaam, na wameahidi kutoa burudani safi kwa wapenzi wa muziki nchini na kuleta ushindani mkubwa katika  tasnia ya muziki nchini.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...