World News

Friday, April 19, 2013

SHOSTEEZ ktk Cover Jarida la MZUKA

Jarida la Mzuka la mwezi April linaloandaliwa na Bongo5 Media Group limetoka huku likiwa na cover story ya kundi jipya la akinadada warembo wa Shosteez.

Katika cover hiyo Shosteez wamefunguka mengi kuanzia jinsi walivyokutana na Lamar, historia ya familia zao na jinsi ambavyo wote wamekua bila kuwa na baba zao, maisha ya ustaa na jinsi wanavyosumbuliwa na wanaume, uhusiano, muziki na mambo mengi kibao.

Pia kuna story kibao kama wanamumuziki wa kike Tanzania wenye mvuto zaidi, mastaa 10 wa kiume Tanzania wanaopiga pamba kali zaidi, madj 10 wa kike Afrika wenye mvuto zaidi, nani aliyeanzisha jina Bongo Flava na historia yake, makosa yanayofanyika kwenye filamu za kibongo na wasichana 8 wapya watakaoupeleka muziki wa Tanzania kimataifa.

Zingine ni pamoja na One on One na Rose Ndauka, Nani zaidi kati ya Sam Misago na B Bozen? (wananchi wameongea). Uchambuzi wa wimbo wa Ney wa Mitego na Diamond – Muziki Gani, Makala kumhusu Navio wa Uganda, bila kusahau Kona ya Mjasiriamali ambapo Patrick Ngowi (mtanzania aliyetajwa na jarida la Forbes miongoni mwa wajasiriliamali bora 30 waliochini ya miaka 30 - 2013) pamoja na picha kali za matukio mbalimbali ya burudani.

Kopi ni shilingi 3,000. Ili kupata nakala yako wasiliana na fred@bongo5.com ama simu 0765537130.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...