World News

Tuesday, June 11, 2013

Pongezi za DefXtro kwa Jambo Squad!

Dx aka DefXtro kama mtayarishaji wa muziki toka Noizmekah Studios nchini Tanzania, nafurahi na pia kujivunia kundi toka Mkoa wa Arusha "Jambo Squad kuibuka washindi wa category ya " Kundi Bora la Muziki wa Kizazi Kipya", Kupitia wimbo wa "Mamong'oo" unaoendelea kutamba zaidi katika Game,Imani imeongezeka kwetu sisi wadau wa muziki tulio mikoani juu ya Uendeshaji wa Tuzo za muziki Tanzania, Changamoto zilizobaki ni jukum letu kama Wazawa kuwasilisha mawazo tutakayozidi kupata kupitia kutazama Tuzo za wenzetu wa nchi zilizoendelea ili tupande ngazi katika maboresho ya Tuzo za Kitanzania. 

Shukrani tele zimwendee Meneja nambari moja Duniani,si mwingine bali ni Mungu Muweza Yote, kwa maana bila uweza wake tusingetambulika kimuziki. Shukrani tele ziwaendee wadau wote wa media mbali mbali wanaotambulisha kazi zetu kwa washabiki na kutupa nafasi ya uwakilishi wa kaskazini Tanzania katika muziki wa Africa kijumla,
 Tungependa kuwa na tuzo za muziki zaidi ya moja chini ya waandaaji na wadhamini wengi tofauti tofauti kitaifa ili kukidhi category za ziada nominations nyongeza ama hata kuleta ushindani zaidi kwa maana idadi ya nyimbo nzuri zinazopewa nafasi na Media mbali mbali hazienei zote kwa pamoja katika Tuzo za Kilimanjaro japo kupitia Tuzo hizi za Kilimanjaro Tanzania Music Awards ni dhahiri kuwa sanaa ya muziki na wasanii wa Tanzania wanazidi kupewa nafasi kama sekta inayoajiri vijana kila kukicha hivyo niombe wadau wengi zaidi kujitokeza kuwekeza katika kuwainua wasanii wa kitanzania hadi kufahamika kimataifa na kutuletea hata tuzo zaidi toka nchi za mbali,
 Noizmekah Studio Itaendelea na punguzo la Bei za kurekodi ili kuboresha tasnia ya muziki wa kizazi kipya Arusha, Tanzania, Africa Mashariki na Duniani kote na kwa mawasiliano zaidi tembelea www.noizmekah.com au piga +255 715 240 005 powered by www.vmgafrica.com

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...