World News

Friday, September 20, 2013

Tamasha la Demokrasia Tanzania


lengo la Tamasha ni kuwaandaa Vijana kuwa Viongozi na kuwajengea hali ya kujiamini jukwaani, kazini, na pia lengo lingine ni kusaidia kupeleka elimu ya Mpiga Kura na ile ya Uraia kwa Jamii, ikiwa ni pamoja na kusaidia kuleta hali ya Utulivu hapa Nchini.

katika Tamasha hilo Wasanii wakongwe wote  wa Muziki, Vichekesho, Sarakasi, na wachezaji maarufu mbalimbali wamealikwa kuhudhuria ambapo kwa  upande wa muziki aina zote za wanamuziki wamealikwa wakiwamo wa miziki ya Bolingo, Kizazi  Kipya, Rage, Taarabu, na michezo yote itaanza mapema asabuhi saa 3:00 na kuendelea, ambapo michezo na maonyesho mengine ambapo wanavyuo wameandaa Dibate Mijadala kwa ajili ya Kuelimisha jamii juu ya Misingi ya Demokrasia na Utawala Bora chini ya Mfumuko wa Vyama Vingi vya Siasa.

Bado tunaendelea na kuomba Wadhamini kujitokeza ili kuweza kufikia malengo isipokuwa waliojitokeza na ambao bado wanaendelea na mazungumzo ni pamoja na BAHATI NA SIBU YA TAIFA, PEPSI, DUME kupitia watu wa Marekani, Tamali Hoteli, CXC Tours & Safari, Tanzania International University(TIU), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM), Dar es Salaam City College, Mama Mtwana Cataring, Nawina Resort Mbagala, 
 
 Nasaha na Ushauri za Miss Demokrasia Tanzania ni pamoja na kuwapa pole  wote wanaoendelea kuwa wagonjwa, wenye matatizo mbalimbali, wajane,  na wanaoendelea kuelemewa na kila aina ya mizigo, kwamba maisha si kuwa na wasiwasi juu ya yote, siku zinavyosogea kuelekea Uchaguzi, kunazidi kuibuka mijadala, na minong;ono kutoka kwa baadhi ya wananchi kwamba pengine hali ya upotvu wa amani unaweza kujitokeza na kuleta machafuko kwa kuwa kumeibuka ushindani mkuu kati ya vyama viwili vya uchaguzi, Chama Tawala CCM ,dhidi ya CHADEMA, Ushauri wetu na nasaha zetu kwako ni kwamba Kikubwa ni kuhakikisha Unatumia Haki yako ya Msingi katika kupiga kura(kuchagua Kiongozi Bora na Siyo Bora Kiongozi).kwa maana akichaguliwa kiongozi kwa kufuata haki na Misingi ya Demokrasia, hakuna Mtu wa Mtanzania yeyote atakayediliki kunyoosha kidole chake kwa maana haki imetumika, Baadhi ya Wananchi wameanza kuweka midomoni mwao Kitu mawazo ya kile  kinachidaiwa na wao kuwa pengine hali ya wasiwasi inazidi kukua siku hadi siku miongoni mwetu kwa kuhofia vita ya sisi kwa sisi itakayosababbishwa na kugombea madaraka. je hayo madaraka wanayogombea ni mali ya Nani? jibu ni wazi tu kwamba ni mali yako wewe ndugu mtanzania, kwa hiyo kumbe ugomvi kama ni kutokea tatizo inakuwa ni sisi na siyo Demokrasia, kwa hiyo tusikubali hata kidogo kutumikia mabwana wawili kwa maana mmoja atakushinda na ndipo hayo yote yanaweza kujitokeza, kile kinaitwa Mapigano(Vita), lakini Kampuni hii ya Miss Demokrasia Tanzania inakuhakikishia kwamba Usiwe na wasiwasi kwa maana hakuna jambo lolote baya litakalojitokeza kwa kuwa watanzania tayari Wamefunguka na wanaendelea kupanuka kifikra na kimawazo, ni wapumbavu wachache sana yaani kikundi cha watu wachache sana ni sawa na asilimia 5 katika 100 wanaowaza na kufikilia Mapambano, Mapigano,na Vita.Zingatia kutoshirikiana na kukubaliana na mawazo ya mtu mpumbavu, mshawishi, mlaghai,Mwivi,Wauaji,usikubali kutoa ama kupokea Rushwa, wakati sasa umefika wa kutambua umuhimu wa haki, uhuru, na kutambua kwamba je ni kwa nini viongozi wanawajibika kwetu kama watumishi? kutambua wajibu wa Viongozi kwa jamii na wajibu wa jamii kwa viongozi,na baada ya kutafakari hayo kumbe je ni kweli kwamba Jamii ndiyo Mwajiri wa Kiongozi wake, je Bosi ni nani kati ya Jamii yaani wewe na Serikali?. je nani anapaswa kumtumia mwenzake? je ukiwa na watoto wagomvi, wezi, wasema uongo, wasiyotii maagizo yako ndani ya nyumba yako  ama ofisini mwako,  nini matarajio yake ya baadae? jitokeze kuunga na kufanikisha juhudi za waandaaji wa TAMASHA LA DEMOKRASIA TANZANIA 2013/15 au unaweza kuwasiliana na wahusika kwa mchango wako, mawazo yako, nia yako, ili tuwe ni wafuasi bora wa imani ya Dini zetu, makabila yetu, na kuhakikisha tunashirikiana kumchagua kiongozi mwadilifu, msikivu, mwenye kulilia maslai ya Umma na mtekelezaji bora wa majukumu ya serikali, atakaye endeleza Muungano na kuhakikisha Tanzania inakuwa ni Taifa Moja lenye Umoja na  Mshikamano kwa ajili ya kulinda na kuhifadhi rasilimali za Taifa, Mistu na Madini, Wanyama, na Ardhi. tupigie simu kwa jambo lolote
+255-713-868209,
+255-713/767-869133
+255-719-592659

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...