World News

Friday, October 25, 2013

Muder Plus Lyrics - Chaba ft. Jordan

Ikiwa bado mixtape yake “Nyota njema ya mtaa” inaendelea kufanya vizuri sokoni, Chaba a.k.a Baba mkubwa anayewakilisha 009 (Ngalimited) Arusha city, anawazawadia wapenzi wa muziki wake track mpya na moto kabisa toka Grandmaster Records chini ya utayarishaji wa producer John B akiwa amemshirikisha Jordan aliyetisha na ngoma yake ya mapenzi vita mapema mwaka huu.
Huyu hapa ni Chaba akiizungumzia track yake mpya;- “Mmmmh! Hii track basically, ni zawadi kwa mashabiki zangu kwa kuipokea vizuri na kuinunua mixtape yangu ili pia wasio nazo waendelee kuinunua, na pia bila kusahau kuwa kawa bado Baba mkubwa nawa-murder rappers wote wanaoigiza sanaa”For Interviews/Bookings; +255713876299


 Lyrics


Track; Murder
Artists; Chaba feat Jordan
Prod;   John B (Grandmaster Records)

Intro;- Kwa hiyo wee ndio jamaa wanamwita akachaba, Mmmmh! Ni nii special kuhusu we jamaa haah! Nini special, well mi nilikuja hapa kuwa-murder!!!!

Verse 1;-

Mistari mara Chaba sawasawa na mchongo,
Ule ambao ukijumlisha wenye akili ubongo,
Basi, unapata jumla ya cash milima, Mgosi wa ndima,
Mama kutoka Meru, Arusha nimesimama juu kuliko Meru,
Balozi wa Rap kutoka mashariki ya Africa, Sihitaji malaika,
Kunilinda kitaa, Nipo na mistari ambayo nikiigawanya haukatiki umeme mitaa,   
Una wivu sababu, Mistari yangu mara doo sawasawa na adhabu,
Kwa yako Career, Wewe ni umbwa unayelia, Nisipokuwepo nikiwepo unafyata mkia,
Basi, Jifunze kuiheshimu yako nafasi,
Huu ni urefu wa kamba hufikii kwa yako kasi, Najumlisha wafuasi,
Nikiwa-murder, Waigiza Hip Hop nakiwazika bila mashada,
Mi ni crazy Baba, Ndoto inayokukata stimu ya miaka saba,
Public figure linalochora miraba,
Isiyohesabika kama pundamilia wote wa Africa na yao miraba,
Unabakia historia kama Nebukalneza, Huu ni muziki wenye sura haijapendeza,
Kama mitaa ambayo serikali imeitelekeza,
Rasmi nipo hapa kuwala MC kama supu ya Pweza!

Chorus x 2 Nakubana tuu kwapani, Kwako nastay,
Nakutia shakani, Naku-murder everyway! Everyway!!
Bridge x 2 Nimechafukwa na roho na hawa mabishoo, Kuja na maswaga kwa Hip Hop show!! Tunawa-murder, (Murder)

Verse 2;-

Sikuanza darasa la kwanza kwanza nilianza, Kuwa MC, Baba mkubwa Macii,
Na nilipogundulika, Kila taa nyekundu ilibadilika kijani,
Mikono ya maproducer ikaanza kunyonga kwa wingi majani, Mabiti yakanitamani,
Kila nilipoyarapia yakaniita Honey,
Zikafa Azonto zikisikia rap zinazochapa viboko, Kwenye mikoko,
Na kwenye vilabu, MaDJ wakatumia rap zangu kimatibabu,
Mpaka nikipita mitaa sasa ikawa balaa, Binti anataka mtoto wangu ili awe staa,
Mi ni jangwa la bahari ya mistari hadimu,
Na ninanyesha madini masika kila msimu,
Haizuiliki, Histori haifunikiki, Tafuteni category kwa hii hamtambuliki,

Chorus x2, Bridge x2, Outro……………………………………{MurdeR!!!!!!!}

John Blass
Grandmaster Audio and video Studio,
+255754201643/892686,
Box 464,
Arusha.
Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...