Profesa Jay akionyesha kwa wanaandishi wa habari (hawapo 
pichani) mfano wa hundi/bango alilokabidhiwa likiwa na Barcode kwa Bidhaa 
yake.
Mwenyekiti wa Bodi ya GS1 Tanzania Bw. Elibariki Mmari (Mwenye 
Koti la suti) akizungumza wakati wa halfa fupi ya kumkabidi Barcode mwanamuziki 
wa Kizazi Kipya Profesa Jay katika makao makuu ya Ofisi hiyo TIRDO Msasani 
jijini Dar Es Salaam, Kulia kwa Bw. Mmari ni Fatma Kange Saleh Afisa Mtendaji 
Mkuu wa GS1 Tanzania na Nd. Pius Mikongoti Afisa Muandamizi toka GS1 Tanzania na 
kushoto kwa Mwenyekiti ni Bw. Joseph Haule aka Profesa Jay.
Wanamuziki nchini wameaswa kuchangamkia fursa zilizopo kwa 
kujitangaza na kutanua wigo wa mashabiki wao kwa kujiunga na huduma ya 
Barcode.
Hayo yamesemwa leo na mwanamuziki Profesa Jay alipokuwa 
akikabidhiwa Barcode za ajili ya CD yake mpya itakayojulikana kama The Best of 
Professor Jay ambayo itakuwa na mchanganyiko wa nyimbo zake ambazo zime heat 
tangu kuanza kwake. “nimeamua kutoka kivingine na kwa sasa nataka kufanya vitu 
kimataifa kwa kusambaza kazi zangu kwenye mitandao ili niwafikie watu wengi 
zaidi” alisema Jay.
Akiongea katika makabidhiano hayo Mwenyekiti wa Bodi ya GS1 
Tanzania Bw. Elibariki Mmari alisema kuwa ni wakati muafaka kwa wanamuziki wa 
Tanznia kuanza kuuza kwenye mitandao ya kijamii na masoko ya kwenye mtandao kama 
wanavyofaidi fursa hizo wanamuziki wengine. Bwana Mmari alisema kuwa kwa kutumia 
fursa hizo wanamuziki hao wanaweza kuuza kwenye mitandao ya kijamii kwa kupitia 
makampuni makubwa duniani kama CD Baby ambalo lina mikataba na maduka yote 
makubwa ya kwenye mtandao kama iTune, Facebook Music na mengine makubwa.
Aidha Mwenyekiti Mmari alitanabaisha kuwa wanamuziki wa 
Tanzania hawawezi kuingia kwenye chati kubwa kama za Billboard bila kuwa na 
utambulisho wa ki electroniki wa Alama za Mistari yaani Barcode. Naye Afisa 
muandamizi wa GS1 Tanzania Bw. Pius Mikongoti alisema kuwa ni vigumu kupata 
takwimu sahihi za usambazaji za wanamuziki wa Tanzania kwani kazi zao haziko 
kwenye mfumo rasmi, “ukiangalia mwanamuziki kama Lady Jay Dee mathalani ana 
wafuasi wamefikia laki moja kwenye mtandao wake wa kijamii wa Facebook kama 
atatangaza kuuza kazi zake kwenye mitandao hiyo ni wazi atawafiukia washabiki 
wake kirahisi zaidi” Takwimu za Billboard zinachukuliwa kutokana na usambazaji 
na mauzo ya kazi za mwanamuziki ki electroniki, ni vigumu kwa mwanamuziki kama 
Diamond ambaye kwa sasa ana mashabiki lukuki na kazi zake kupigwa kila kona 
kupata takwimu sahihi za usambazaji wake.
Aidha amewataka wadau wa muziki nchini kuacha kusambaza nyimbo 
mpya za wanamuziki kwenye mitandao na kuwafanya watu waweze kuzipata bila 
kuzitolea chochote (downloads), kwa kufanya hivyo tunawaumiza wanamuziki na 
tunakuwa hatuwasaidiii aliongeza Bw. Mikongoti. GS1 Tanzania ndio watoaji pekee 
wa huduma za BArcode kwa bidhaa zote za Tanzania, ikumbukwe kuwa ili uweze kuuza 
kwenye Supermarket na masoko ya mitandaoni ni lazima uwe na alama hizi za 
mistari yaani Barcode.

No comments:
Post a Comment