Thursday, October 9, 2014

WAMAMA ZAIDI YA 50 KUFAIDIKA NA TAMASHA LA UPENDO

Ndani ya mwezi ujao wa Kumi na Moja (November) Tarehe 2 itakuwa ni siku yenye Neema kwani Arusha Kutashushwa Baraka ya Kumthamini na kumuonyesha Upendo Mama Wa Kitanzania na Duniani Kote.

Hadi sasa Maandalizi ya Tamasha la Upendo kwa Mama Yamekamilika ambapo Tarehe 2 November 2014 Ndani ya Viwanja vya Sheikh Amri Abeid Kutafanyika tamasha hilo lililobarikiwa jina la UPENDO KWA MAMA ambapo Tamasha hilo litaongozwa na waimbaji wa Nyimbo za Injili wakubwa kutoka humu Nchini na Nchi Jirani ya Kenya.
 
Wasanii hao wa Injili Watakaoongoza Tamasha la UPENDO KWA MAMA Sara K kutoka Nchini Kenya na Cristina Shusho kutoka Tanzania, huku likipambwa na Ambwene Mwasongwe, Baraka Maasa, Eng calros Mkundi, Ester Bukuku, Matha Mwaipaja, Nesta sanga, Meth Chengula, Matumaini, Eline Patrick bila kuwasahau waimbaji wengine kutoka Mkoani Arusha pamoja na Kwaya Mbalimbali.

Lengo hasa la tamasha hilo la UPENDO KWA MAMA ni kutoa Mitaji kwa zaidi ya akina mama 50 wajasiriamali ili kuwaongezea uwezo wa kujiajiri, vilevile utakuwa ni wakati mwafaka wa kuwashukuru wakinamama wote kwa upendo walionao ukiambatana na kujitolea katika kusimamia Familia na malezi ya watoto.
 
Kama Mtanzania au Usiyekuwa Mtanzania mwenye Mapenzi na mama Basi unaalikwa Kufika katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha Tarehe hiyo na utashuhudia Tamsha hilo kwa Kuchangia Kiingilio Kidogo tu ambacho ni Sh. 3,000/= (Elfu Tatu ya Kitanzania)

Tamasha la UPENDO KWA MAMA limeandaliwa na Mkundi Production ya Jijini Arusha na wao kama kamati ya maandalizi ya Tamasha la UPENDO KWA MAMA wanatoa nafasi kwa watanzania, Taasisi na Mashirika yote ambayo yako tayari kuungana na Studio ya Mkundi kwa Ufadhili wa hali na mali ili kufanikisha tamasha hili la UPENDO KWA MAMA.

No comments:

Post a Comment