Mkurugenzi wa Wilaya ya Mkuranga akiongea na wasanii baada ya kuwakaribisha ktk kijiji cha Ngarambe yalipo mashamba yao na kuwaasa kuwa wachapakazi sawasawa na Baba wa Taifa alivyokuwa mchapakazi kwa vitendo. Hali kadhalika Mkurugenzi huyo aliwaomba wasanii wafanye kweli ili mashamba yao yawe mfano kwa wakazi wote wa Mkuranga.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Wasanii (SHIWATA) akiongea na waandishi wa habari Siku hiyo ya kumkumbuka Baba wa Taifa ktk mashamba ya wasanii Ngarambe huko Mkuranga mkoa wa Pwani. Ktk maongezi yake m/kiti alisema kwamba SHIWATA imenunua ekari 500 za shamba ktk kijiji cha Ngarambe, ila mpaka sasa wamejitokeza wasanii 95 tu ambao ndio wenye nia ya kulima na wote wamekabidhiwa ekari zao ktk shamba hilo tayari kwa Kilimo cha Kisasa. SHIWATA ina wanachama 8000 kwa sasa.
Vijana wa kijiji cha Ngarambe wakiwa ktk pilika za kuwasaidia wasanii kuandaa sound na vitu vingine kuathimisha Nyerere day!
Kiongozi wa dini ya kiislamu hapo kijijini akiongea na wasanii sambamba na kupiga Dua ktk siku hiyo
Mkuu wa Tarafa ambae pia alimuwakirisha Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga akiongea na kuwakaribisha wasanii ktk mashamba ya Ngarambe, kata ya Ngarambe kuu.
Afisa Kilimo wa wilaya naye aliongea na wasanii na kuwaasa juu ya Kilimo bora
Muwakilishi wa Ofisi ya Vijana, Utamaduni na Michezo ambaye pia ni Katibu wa SHIWATA akiongea na viongozi ktk meza kuu pamoja na wasanii waliofika ktk mashamba ya Ngarambe
Kiongozi wa BASATA naye alikuwepo ktk mashamba hayo sambamba na kumuenzi Baba wa Taifa
Baadae wasanii walikabidhiwa mashamba pamoja na cheti cha umiliki wa umiliki wa shamba ktk ekari 500 za Shamba la SHIWATA
No comments:
Post a Comment