World News

Wednesday, October 22, 2014

'YP' KUZIKWA CHANG'OMBE LEO JIONI!!

Marehemu Yesaya Ambilikile 'YP', msanii wa kundi la TMK Wanaume Family alizaliwa tar 10/11/1986, anatarajiwa kuzikwa leo jioni kwenye makaburi ya Chang'ombe Maduka Mawili. Mwili wake unategemewa kuagwa ktk viwanja vya Sigara Changombe leo mchana 


Msanii huyo alifariki usiku wa kuamkia jana ktk hospitali ya Temeke kutokana na kusumbuiliwa na maradhi ya kifua kwa muda mrefu.

Marehemu YP aliyewahi kutamba na nyimbo 'Ulipenda pesa', 'Pumzika km huziwezi pombe' 'Shamsa' akiwa na msanii mwenzake Y Dash na zingine alizofanya na TMK Wanaume kama 'Twende Zetu', 'Tufurahi', Dar Mpaka Moro, 'Umri' nakadhalika.

Bwana ametoa na ametwaa Jina lake lihimidiwe!
Neema ya milele umpe ee bwana na mwanga wa milele umwangazie!
Apumzike kwa Amani!

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...