Pages

Wednesday, November 12, 2014

AMINI afata nyayo za LINAH.... Aaachana na MBELEKO ya THT

Msanii AMINI MWINYIMKUU ameachia nyimbo yake mpya inayoitwa MBELEKO punde baada ya kutoka katika jumba la vipaji vya muziki Tanzania THT ambapo alidumu hapo kwa takribani MIAKA 9 na sasa anafanya kazi na kampuni ya BME.

Amini atakuwa msanii wa pili kutoka THT kwenda kufanya kazi na kampuni nyingine awali mwezi Julai mwaka huu msanii mwingine Linah Sanga aliachana na THT na sasa yupo chini ya 'NFZ' No Fake Zone ya Afrika Kusini.
BOFYA kusikiliza MBELEKO 

No comments:

Post a Comment