World News

Tuesday, December 23, 2014

'SONGA' ANAONGOZA KWA DOWNLOAD NYINGI ZA HIPHOP BONGO - MDUNDO

Mdundo ni kampuni ya kimtandao inayojiusisha na usambazaji wa muziki kwa nchi za Afrika Mashariki na makao makuu ni Mdundo ilianzishwa na waanzilishi wawili ambao ni Francis Amisi na Martin Nielsen.Mkurugenzi mkuu wa Mdundo Martin Nielsen amesema kwa sasa wana mkusanyiko wa nyimbo zaidi ya 20,000 na huku wakiteka soko la muziki kwenye nchi 11.Mdundo inapata pesa kupitia kwenye kampuni ambazo zinatangaza kwao kama Microsoft, Samsung na Nokia na huku wasanii zaidi ya 600 wakijiunga.
Kwenye orodha ya wasanii 10 ambao nyimbo zao zimepakuliwa zaidi ni;
1.SAUTI SOL
Kundi hili la Kenya linawjumuisha wasanii Bien-Aime Baraza, Willis Austin Chimano, Savara Mudigi na Polycarp Otieno linaongoza kwa nyimbo zao kupakuliwa kwenye Mdundo kwa 2014.Kundi hili lina nyimbo matata kama Sura yako,gentleman na money lover.

141202104055-sauti-sol-mdundo-horizontal-gallery
2.JUX
Msanii huyu wa RNB anaetesa kwa nyimbo ya “Uzuri wako” anashikilia nafasi ya pili kwenye nyimbo zinazopakuliwa kwa wingi kwa nyimbo za Afrika Mashariki.

141204123032-jux-mdundo-horizontal-gallery
3.ELANI
Kundi hili la Kenya linatesa kwa nyimbo ya Milele na nyingine nyingi inashika nafasi ya tatu kwa Afrika Mashariki.

141202104100-elani-mdundo-horizontal-gallery
4.SIZE 8
Msanii huyu wa kike wa Kenye licha ya kuhamia kwenye muziki wa Dini ila nyimbo zake zinaongoza kwa kupendwa na wapenzi wa muziki kwenye pande ya Afrika Mashariki na anatesa kwa nyimbo yake ya “Tamtam remix”.

size-8
5.BAHATI
Msanii huyu tokea pwani ya Kenya anatesa na kibao kinachoitwa “Siki ya Kwanza” na pia anshikilia tuzo saba ikiwemo msanii bora wa kiume kutoka pwani.

141202104105-bahati-mdundo-horizontal-gallery

6.H ART THE BAND
Kundi hili linaloundwa na wasanii Wachira Gatama, Kenneth Muya- Kenchez na Mordecai Mwini linaongoza kwa sauti nzuri,mashari.

141202104108-h-art-the-band-mdundo-horizontal-gallery

7.JAGUAR
Msanii huyu wa nyimbo ya ‘Kioo’ anaonekana kuendelea kutesa kwa mbali swaiba wake wenye upinzani Prezzo.

jaguar

8.RABBIT KAKA SUNGURA
Msanii huyu wa Kenya ambaye alitoa albumu yake ya kwanza mwaka 2008 anaonekana kutikisa kwenye muziki wa Hip-Hop na kuwafunika kwa mbali wasanii wenzake wa Hip Hop nchini Kenya.

141202104114-rabbit-mdundo-horizontal-gallery

9.NAMELESS
Msanii huyu wa kibao cha “Coming Home’ anatikisa kwenye soko la muziki Afrika mashariki hasa vibao vyake vilivyotesa kote Duniani kama Nasinzia Nikikuwaza,Butterfly na Ninanoki.

141202104116-nameless-mdundo-horizontal-gallery

10.SONGA
Msanii huyu anaetokea kwenye kundi la “Tamaduni Music” licha ya kutoteka sana soko la muziki nchini Tanzania ila anaongoza kwa baadhi ya nyimbo zake kupakuliwa zaidi na kuwakimbiza wasanii wengine wa Hip-Hop nchini Tanzania,baadhi ya nyimbo zinazopendwa na mashabiki na hivyo kupelekea kuwepo kwenye no. 10 ya nyimbo bora kwa mwaka 2014 ni Usiku,Niite Songa,Ndege na Sorry.

141202104119-songa-mdundo-horizontal-gallery
Source; Hivisasa

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...