Mdundo ni kampuni ya kimtandao
inayojiusisha na usambazaji wa muziki kwa nchi za Afrika Mashariki na
makao makuu ni Mdundo ilianzishwa na waanzilishi wawili ambao ni Francis
Amisi na Martin Nielsen.Mkurugenzi mkuu wa Mdundo Martin Nielsen
amesema kwa sasa wana mkusanyiko wa nyimbo zaidi ya 20,000 na huku
wakiteka soko la muziki kwenye nchi 11.Mdundo inapata pesa kupitia
kwenye kampuni ambazo zinatangaza kwao kama Microsoft, Samsung na Nokia
na huku wasanii zaidi ya 600 wakijiunga.
Kwenye orodha ya wasanii 10 ambao nyimbo zao zimepakuliwa zaidi ni;
1.SAUTI SOL
Kundi hili la Kenya linawjumuisha wasanii Bien-Aime Baraza, Willis
Austin Chimano, Savara Mudigi na Polycarp Otieno linaongoza kwa nyimbo
zao kupakuliwa kwenye Mdundo kwa 2014.Kundi hili lina nyimbo matata kama
Sura yako,gentleman na money lover.
2.JUX
Msanii huyu wa RNB anaetesa kwa nyimbo ya “Uzuri wako” anashikilia
nafasi ya pili kwenye nyimbo zinazopakuliwa kwa wingi kwa nyimbo za
Afrika Mashariki.
3.ELANI
Kundi hili la Kenya linatesa kwa nyimbo ya Milele na nyingine nyingi inashika nafasi ya tatu kwa Afrika Mashariki.
4.SIZE 8
Msanii huyu wa kike wa Kenye licha ya kuhamia kwenye muziki wa Dini ila
nyimbo zake zinaongoza kwa kupendwa na wapenzi wa muziki kwenye pande ya
Afrika Mashariki na anatesa kwa nyimbo yake ya “Tamtam remix”.
5.BAHATI
Msanii huyu tokea pwani ya Kenya anatesa na kibao kinachoitwa “Siki ya
Kwanza” na pia anshikilia tuzo saba ikiwemo msanii bora wa kiume kutoka
pwani.
6.H ART THE BAND
Kundi hili linaloundwa na wasanii Wachira Gatama, Kenneth Muya- Kenchez na Mordecai Mwini linaongoza kwa sauti nzuri,mashari.
7.JAGUAR
Msanii huyu wa nyimbo ya ‘Kioo’ anaonekana kuendelea kutesa kwa mbali swaiba wake wenye upinzani Prezzo.
8.RABBIT KAKA SUNGURA
Msanii huyu wa Kenya ambaye alitoa albumu yake ya kwanza mwaka 2008
anaonekana kutikisa kwenye muziki wa Hip-Hop na kuwafunika kwa mbali
wasanii wenzake wa Hip Hop nchini Kenya.
9.NAMELESS
Msanii huyu wa kibao cha “Coming Home’ anatikisa kwenye soko la muziki
Afrika mashariki hasa vibao vyake vilivyotesa kote Duniani kama Nasinzia
Nikikuwaza,Butterfly na Ninanoki.
10.SONGA
Msanii huyu anaetokea kwenye kundi la “Tamaduni Music” licha ya kutoteka
sana soko la muziki nchini Tanzania ila anaongoza kwa baadhi ya nyimbo
zake kupakuliwa zaidi na kuwakimbiza wasanii wengine wa Hip-Hop nchini
Tanzania,baadhi ya nyimbo zinazopendwa na mashabiki na hivyo kupelekea
kuwepo kwenye no. 10 ya nyimbo bora kwa mwaka 2014 ni Usiku,Niite
Songa,Ndege na Sorry.
No comments:
Post a Comment