Bendi ya muziki INAFRIKA BAND aka "Wazee wa Indege" kutoka jiji Dar,ilifanikiwa kulitingisha jiji la Bremen,nchini Ujerumani katika
onyesho liliofanyika usiku wa 13 Februari 2015 katika ukumbi mkubwa wa
Musik-Theater mjini Bremen,Ujerumani,ambako bendi hiyo kutoka
Chang'ombe ilisimama jukwaani na kuziteka nyoyo za maelfu ya wapenzi wa
muziki, aidha bendi ya Inafrika bend imetajwa kuwa bendi bora
ya muziki wa Folk na radio Funkhaus-Europe.
Vionjo vya mitindo ya
muziki wa asili wa makabila ya kitanzania vilivyotumiwa na Inafrika Band
katika kuteka yonyo za washabiki kila kuona duniani. Inafrika Band
imefanikiwa kuliweka jina ala Tanzania katika tufe la dunia kwa kutumia
mitindo yake ya vionjo vya kiasilia.
Inafrika Band ndio bendi
kwanza yenye makao Tanzania inayoongoza kufanya tour ndefu duniani
wameshafanya ziara katika mabara yote duniani kuanzia
Afrika,Austaria,Amerika,Asia ,Europe na visiwa vya Karebiki.
Wakali
hawa wa mdundo inayokubalika kimataifa wanatisha na kuzoa washabiki kwa
dhoruba kali la mtindo wao wa muziki. Inafrika band inatuwakilisha bado
wapo katika ziara ndefu na wanahakikisha kuwa muziki wao unasikika
kila kona nje ya mipaka ya kimataifa.
msikose kuwasikiliza Inafrika Band (Wazee wa Indege) at http://www.inafrikaband.co. tz pia wape hi at info@inafrikaband.co.tz ii
No comments:
Post a Comment