Africa Unite Party Jumamosi 14 March 2015
Bendi ya maarufu Ngoma Africa Band aka FFU-Ughaibuni aka Anunaki aliens
Bendi ya maarufu Ngoma Africa Band aka FFU-Ughaibuni aka Anunaki aliens
bendi
hiyo inatarajiwa kutumbuiza katika onyesho maalumu la AFRICA UNITE
PARTY litakalofanyika katika ukumbi wa VTS uliopo mtaa wa Augusburger
Str.442 D-70327 mjini Stuttgart,nchini Ujerumani.Onyesho hilo
limeandaliwa
na shirika la Afrikaktiv e.V wakishirikiana na shirika la Cabaret du Monde,
Ngoma Africa band iliyozoeleka kwa kuwatia kiwewe washabiki wake kila
kona duniani wataporomosha muziki moto moto na mdundo wao maarafu
kama " Extraordinary Bongo Dansi" mdundo unaotingisha bila ya kuwa na
mpinzani huko ughaibuni, bendi hiyo inadumu katika medani ya muziki kwa
muda wa miaka 23 na kufanikiwa kujizolea washabiki kila kona.
Ticket za onyesho hilo zinapatikana kwa simu ( booking): Call9+49 0)152 12091242 au +49(0)152 106106137 Mnakaribishwa wote,pia usikose kuwasikiliza
FFU-Ughaibuni at www.ngoma-africa.com
No comments:
Post a Comment